51. Mwenye kumuomba Mtume ambaye kishakufa amemuabudu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mwambie: “Ikiwa umekubaliana na mimi ya kwamba ni ´ibaadah na unamuomba Allaah usiku na mchana, kwa khofu na unyenyekevu, kisha ukaomba kwa haja hiyo Mtume au asiyekuwa yeye; je utakuwa umeshirikisha katika ´ibaadah ya Allaah mwengine asiyekuwa Yeye?” Hana budi kusema: “Ndio.”

MAELEZO

Baada ya kumbainishia kuwa du´aa ni ´ibaadah na akakubali, basi mwambie:

“Je, utakuwa si mwenye kumuabudu mwengine asiyekuwa Allaah endapo utatumbukia katika haja na ukamuomba Allaah (´Azza wa Jall) kisha ukamuomba Mtume au mtu mwingine haja hiyohiyo?” Hana budi kusema: “Ndio.”, ni vigumu kukwepa uhakika huu.

Haya ni kuhusiana na du´aa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 67
  • Imechapishwa: 24/11/2023