Kuwatengenezea chakula wafiliwa ni katika mazuri ya Shari´ah ambayo amekuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayahi wa sallam). Wafiliwa hawatakiwi kujikalifisha kumtengenezea chakula yeyote. Kinyume chake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayahi wa sallam) amewaamrisha watu kuwatengenezea chakula wafiliwa. Hii ni moja katika tabia na sifa tukufu zaidi. Kitendo kama hichi kinawasahilishia wale wafiliwa na kuzitia nguvu nyoyo zao. Msiba wao umewashughulisha kutokamana na kujitengenezea chakula wao wenyewe. Mtu asemeje kuwatengenezea chakula wengine na kuwajali? Wafiliwa wanastarehe kwa njia mbili pindi wanapotengenezewa chakula:

Ya kwanza: Watashughulika na yule maiti, kumwandaa, kumuosha, kumvisha sanda, kumswalia swalah ya jeneza, kumbeba na kumzika. Haya yanatosheleza kwa wao kujishughulisha na watu.

Ya pili: Hawali khasara. Yanawasahilishia wale wafiliwa. Leo hii kabla ya maiti kuwahi kuzikwa kunapotea pesa nyingi. Kwa hiyo kusikusanyike khasara mbili.

Kumethibiti dalili katika Sunnah juu ya kuwatengenezea chakula wafiliwa, sawa ikiwa yule maiti alikuwa safarini au mkazi wake au sawa ikiwa wale wafiliwa watapatwa na khasara au hawapatwi na khasara. Kuna bishara kwa yule mwenye kuwatengenezea chakula na kuwapelekea. Atayefanya hivo atakuwa amefuata Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kujisalimisha na maamrisho yake. Imaam Ahmad amepokea katika “al-Musnad” yake kupitia kwa ´Abdullaah bin Ja´far (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Pindi taarifa ya kuuawa kwa Ja´far (Radhiya Allaahu ´anh) ilipofika, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: “Watengenezeeni chakula familia ya Ja´far! Hakika wamefikwa na jambo lenye kuwashughulisha.”

Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah.

Imepokelewa kuwa ´Abdullaah bin Abiy Bakr amesema:

“Sunnah hii haikuacha kuendelea kuwa kati yetu mpaka ikaachwa na wenye kuiacha.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 19/10/2016