Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

43 – Madai yote ya unabii baada yake ni upotofu na kuchupa mipaka.

MAELEZO

Haya yameshatangulia kubainishwa. Madai yote ya unabii baada yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni ukafiri na batili. Hatokuja Nabii mwingine baada ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati ataposhuka katika zama za mwisho hatokuja akiwa kama Nabii au Mtume au kuja na Shari´ah mpya. Hakika si venginevyo atakuja akiwa kama mwenye kuifanya upya dini ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mwenye kumfuata na atahukumu kwa Shari´ah ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 64
  • Imechapishwa: 09/12/2022