8 – ´Umar bin Muhammad ameeleza kwamba baba yake amemweleza kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd bin ´Amr bin Nufayl ambaye amesema:

”Arwaa alizozana naye juu ya baadhi ya ardhi zake ambapo akasema: ”Mwache na baba yake. Kwani hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Yule ambaye atachukua shubiri moja ya ardhi pasi na haki, basi atabebeshwa ardhi saba siku ya Qiyaamah.”

Ee Allaah! Ikiwa ni mwongo basi pofusha macho yake na lifanye kaburi lake nyumbani kwake.” Baadaye nikamuona akiwa kipofu, akijisaidia kwa ukuta, akisema: ”Nimepatwa na du´aa ya Sa´iyd bin Zayd.” Wakati alipokuwa anatembea nyumbani akatumbukia ndani ya kisima kilichokuwa nje ya nyumba yake. Kikawa ndio kaburi lake.”[1]

[1] Muslim (1610).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 27/09/2023