Swali: Je, inafaa kuswali Tarawiyh nyuma ya imamu anayesoma Qur-aan haraka sana kiasi cha kwamba kisomo chake hakiko wazi? Pamoja na kuzingatia kwamba hatuna imamu mwingine.
Jibu: Imamu anapasa kuisoma Qur-aan kwa utaratibu ipasavyo. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا
“Soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu na utungo.”[1]
Qur-aan namna hii haitakikani kwa sababu hakupatikani ndani yake mazingatio. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Usisome Qur-aan haraka sana kama mashairi, na usiitawanye kama tende mbovu. Simama katika maajabu yake na itikise kwayo nyoyo.”[2]
Kwa sababu makusudio ya kisomo cha Qur-aan ni mazingatio maana yake na kuwanufaisha wasikilizaji. Kusoma kwa haraka sana inaweza kupelekea kuondosha baadhi ya herufi zake na kutonufaika wale wafuatiliaji. Kwa ajili hiyo imamu huyu anatakiwa kunasihiwa na kujuzwa kuwa malengo ya kisomo cha Qur-aan ni kuzingatia na kuelewa, na sio tu kisomo cha haraka ambacho kinaishilia haraka na pengine kikaharibu maana na wasifaidike wale wasikilizaji walioko nyuma.
[1] 73:4
[2] Ibn Abiy Shaybah (8833).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 39-40
- Imechapishwa: 04/04/2022
Swali: Je, inafaa kuswali Tarawiyh nyuma ya imamu anayesoma Qur-aan haraka sana kiasi cha kwamba kisomo chake hakiko wazi? Pamoja na kuzingatia kwamba hatuna imamu mwingine.
Jibu: Imamu anapasa kuisoma Qur-aan kwa utaratibu ipasavyo. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا
“Soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu na utungo.”[1]
Qur-aan namna hii haitakikani kwa sababu hakupatikani ndani yake mazingatio. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Usisome Qur-aan haraka sana kama mashairi, na usiitawanye kama tende mbovu. Simama katika maajabu yake na itikise kwayo nyoyo.”[2]
Kwa sababu makusudio ya kisomo cha Qur-aan ni mazingatio maana yake na kuwanufaisha wasikilizaji. Kusoma kwa haraka sana inaweza kupelekea kuondosha baadhi ya herufi zake na kutonufaika wale wafuatiliaji. Kwa ajili hiyo imamu huyu anatakiwa kunasihiwa na kujuzwa kuwa malengo ya kisomo cha Qur-aan ni kuzingatia na kuelewa, na sio tu kisomo cha haraka ambacho kinaishilia haraka na pengine kikaharibu maana na wasifaidike wale wasikilizaji walioko nyuma.
[1] 73:4
[2] Ibn Abiy Shaybah (8833).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 39-40
Imechapishwa: 04/04/2022
https://firqatunnajia.com/49-imamu-anaswali-tarawiyh-haraka-sana/