Anapoanza kusoma, hali yake iwe ni unyenyekevu na kutafakari wakati wa kusoma. Dalili zake ni nyingi kuliko kuweza kuhesabiwa, mashuhuri na dhahiri zaidi kuliko kuhitaji kutajwa. Hilo ndilo kusudio linalotakiwa. Kwa hilo vifua hufunguka na nyoyo hung’aa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا
“Je, kwa nini hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiye Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.”[1]
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ
“Kitabu Tumekiteremsha kwako hali ya kuwa chenye baraka ili wapate kuzingatia kwa makini Aayah zake na ili wapate kukumbuka wale wenye akili.”[2]
Hadiyth kuhusu hili ni nyingi, maneno ya Salaf juu yake ni yenye kutambulika. Jopo la Salaf walikuwa wakikesha usiku wakisoma Aayah moja, wakiitafakari na kuiirudia mpaka asubuhi. Baadhi ya Salaf walikuwa wakizimia wakati wa kusoma. Wengine walifariki wakiwa katika hali ya kusoma. Tumesimuliwa kutoka kwa Bahz bin Hakiym kwamba Zuraarah bin Awfaa, mwanafunzi mtukufu wa Maswababah (Radhiya Allaahu ´anh), aliwaongoza watu katika swalah ya Fajr, akasoma mpaka alipofikia Aayah:
فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ
”Basi hiyo itakuwa ni siku ngumu. Kwa makafiri si nyepesi.”[3]
akaanguka na kufariki. Bahz amesema:
”Nami nilikuwa miongoni mwa waliombeba.”
Ahmad bin Abiyl-Hawaariy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye kwa mujibu wa Abul-Qaasim al-Junayd (Rahimahu Allaah), alikuwa ni ua la Shaam, Qur-aan ikisomwa mbele yake, alikuwa akipiga kelele na kuanguka. Ibn Abiy Daawuud amesema:
”al-Qaasim bin ´Uthmaan al-Juw´iy (Rahimahu Allaah) alikuwa akimpinga Ibn Abiyl-Hawaariy kwa hilo. al-Juw´iy alikuwa mtu mwenye fadhilah katika wanazuoni wa Hadiyth wa watu wa Dameski na alikuwa mbele kwa ubora kuliko Ibn Abiyl-Hawaariy… Abul-Jawzaa´, Qays bin Habtar na wengineo walimpinga kwa jambo hilo.”
Maoni sahihi ni kutokukataza isipokuwa kwa yule anayetambulika kuwa anafanya hivyo kwa kujifanya – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
Kiongozi mtukufu, mwenye vipawa na maarifa, Ibraahiym al-Khawwaasw (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Dawa ya moyo ni mambo matano: Kusoma Qur-aan kwa mazingatio, kupunguza chakula, kusimama usiku kuswali, kujinyenyekeza wakati wa mwisho wa usiku na kukaa pamoja na watu wema.”
[1] 4:82
[2] 38:29
[3] 74:9-10
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 55
- Imechapishwa: 31/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 55
Imechapishwa: 31/08/2026
https://firqatunnajia.com/48-unyenyekevu-wakati-wa-kusoma-qur-aan/