47. Kuanza kwa jina la Allaah kabla ya kusoma Qur-aan

Mwanzoni mwa kila Suurah, isipokuwa tu Baraa-ah, anapaswa kutilia umuhimu kusema:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

“Kwa jina la Allaah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”

Kwani wanazuoni wengi wameona kuwa ni Aayah inapokuwa imeandikwa katika msahafu. Imeandikwa mwanzoni mwa kila Suurah isipokuwa tu Baraa-ah, hivyo akiisoma anakuwa na yakini ya kusoma hitimisho au Suurah kamili. Akiacha Basmalah, basi anakuwa ameacha sehemu ya Qur-aan kwa mujibu wa wanazuoni wengi.

Ikiwa kusoma ni katika mgawo maalum uliopangwa kama sehemu zilizo na Waqf au malipo, basi kuzingatia Basmalah kunakuwa muhimu zaidi ili kuwa na yakini ya kukamilisha hitimisho. Kwani akiiacha, hastahiki chochote katika Waqf kwa yule mwenye kuona kuwa Basmalah ni Aayah mwanzoni mwa Suurah. Hili ni jambo makini na lenye faida kubwa ambalo linapaswa kuzingatiwa na kuenezwa.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 31/08/2026