Ikiwa anataka kuanza kusoma Qur-aan, basi aombe kinga na kusema:
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم
”Najilinda kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa.”
Hivi ndivyo walivyosema wengi wa wanazuoni. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuomba ulinzi hufanywa baada ya kusoma, kwa sababu ya Amesema (Ta´ala):
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
“Unapotaka kusoma Qur-aan basi, omba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”[1]
Makusudio ya Aayah hii kwa mujibu wa wengi wa wanazuoni:
”Unapokusudia kusoma Qur-aan, basi mtake hifadhi Allaah dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa.”
Namna ya kutaka kinga ni kama ilivyotajwa hapo juu. Salaf wengi walikuwa wakisema:
أَعوذ بالله السميع العليم من الشَّيْطانِ الرَّجِيمِ
”Najilinda kwa Allaah, Msikivu, Mjuzi, kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa.”[2]
Hili halina ubaya, lakini chaguo lililo bora ni lile la kwanza.
Kisha kuomba kinga ni jambo linalopendeza na si wajibu. Inapendekezwa kwa kila msomaji, ni mamoja awe ndani ya swalah au nje ya swalah. Kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi kati ya maoni mwili ya wafuasi wetu ni kuwa inapendeza katika kila Rak´ah. Maoni ya pili yanasema kuwa inapendeza tu katika Rak´ah ya kwanza; ikiachwa katika Rak´ah ya kwanza basi itasomwa katika Rak´ah ya pili. Aidha inapendeza kuomba kinga dhidi ya shaytwaan katika Takbiyr ya kwanza katika swalah ya jeneza kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya madhehebu kati ya maoni mawili.
[1] 16:98
[2] Abu Daawuud (775) na at-Tirmidhiy (242). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (106).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 54
- Imechapishwa: 31/08/2026
Ikiwa anataka kuanza kusoma Qur-aan, basi aombe kinga na kusema:
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم
”Najilinda kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa.”
Hivi ndivyo walivyosema wengi wa wanazuoni. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuomba ulinzi hufanywa baada ya kusoma, kwa sababu ya Amesema (Ta´ala):
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
“Unapotaka kusoma Qur-aan basi, omba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”[1]
Makusudio ya Aayah hii kwa mujibu wa wengi wa wanazuoni:
”Unapokusudia kusoma Qur-aan, basi mtake hifadhi Allaah dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa.”
Namna ya kutaka kinga ni kama ilivyotajwa hapo juu. Salaf wengi walikuwa wakisema:
أَعوذ بالله السميع العليم من الشَّيْطانِ الرَّجِيمِ
”Najilinda kwa Allaah, Msikivu, Mjuzi, kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa.”[2]
Hili halina ubaya, lakini chaguo lililo bora ni lile la kwanza.
Kisha kuomba kinga ni jambo linalopendeza na si wajibu. Inapendekezwa kwa kila msomaji, ni mamoja awe ndani ya swalah au nje ya swalah. Kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi kati ya maoni mwili ya wafuasi wetu ni kuwa inapendeza katika kila Rak´ah. Maoni ya pili yanasema kuwa inapendeza tu katika Rak´ah ya kwanza; ikiachwa katika Rak´ah ya kwanza basi itasomwa katika Rak´ah ya pili. Aidha inapendeza kuomba kinga dhidi ya shaytwaan katika Takbiyr ya kwanza katika swalah ya jeneza kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya madhehebu kati ya maoni mawili.
[1] 16:98
[2] Abu Daawuud (775) na at-Tirmidhiy (242). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (106).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 54
Imechapishwa: 31/08/2026
https://firqatunnajia.com/46-kuomba-ukinga-dhidi-ya-shaytwaan-kabla-ya-kuanza-kusoma-qur-aan/