Inapendekezwa kwa msomaji wa Qur-aan nje ya swalah kuelekea Qiblah. Kwani imekuja katika Hadiyth:
”Vikao vilivyo bora ni vile vinavyoelekezwa Qiblah.”[1]
Aidha akae kwa unyenyekevu hali ya kuwa mtulivu na mwenye heshima, akiwa ameinamisha kichwa chake. Akae peke yake kwa namna inayokamilisha adabu yake na unyenyekevu wake, kama anavyokaa mbele ya mwalimu wake. Hii ndiyo hali iliyo bora zaidi.
Ikiwa atasoma hali ya kuwa amesimama, amelala ubavuni, juu ya kitanda chake au katika hali nyingine yoyote, inajuzu na atapata ujira. Hata hivyo hali hiyo ni chini ya ile ya kwanza. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
”Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni ishara kwa wale wenye akili; ambao wanamtaja Allaah hali ya kuwa wima, wamekaa au wamejinyoosha na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi [wakisema]: ”Mola wetu, Hukuumba haya bure, utakasifu ni Wako! Basi Tulinde na adhabu ya Moto.”[2]
´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiegemea mapajani mwangu hali mimi nina hedhi na anasoma Qur-aan.”[3]
Ameipokea na al-Bukhaariy na Muslim. Imekuja katika riwaya nyingine:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anasoma Qur-aan huku kichwa chake kikiwa mapajani mwangu hali mimi nina hedhi.”
Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Hakika mimi nasoma Qur-aan ndani ya swalah yangu na nasoma nikiwa kitandani mwangu.”

”Hakika mimi husoma sehemu yangu ya kila siku nikiwa nimelala juu ya kitanda.”
[1] Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3085).
[2] 3:190-191
[3] al-Bukhaariy (297), Muslim (301) na Abu Daawuud (260).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk.
- Imechapishwa: 31/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk.
Imechapishwa: 31/08/2026
https://firqatunnajia.com/45-vikao-vya-kisomo-cha-qur-aan/