Hadiyth hii ni dalili kwamba mwenye kufanya kitendo kilichoharamishwa na hajatambua hukumu ya Kishari´ah, basi ni juu yake kuwauliza wanazuoni kuhusu alichofanya kinyume na Shari´ah na aogope matokeo mabaya ya kitendo chake. Hili lina mfano wake katika kisa cha al-´Asayf, kisa cha Maa´iz (Radhiya Allaahu ´anh) na vinginevyo.
Wanazuoni wengi wametumia dalili kwa maneno yake:
“Nimeangamia.”
kwamba alikuwa akilijua jambo hilo na kwamba alikuwa akifahamu uharamu wake. Vilevile kilichokuja katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwa al-Bukkhaariy na Muslim kwamba alisema:
“Nimeungua.”
Kwa sababu kuangamia na kuungua ni istilahi ya kufananisha madhambi yanayoweza kusababisha hayo. Wamesema kwamba haingii katika hukumu hiyo aliyesahau wala mjinga wa hukumu. Basi mwenye kujamiiana kwa kusahau au kwa kutojua, basi hana jukumu la kulipa wala kutoa kafara. al-Bukhaariy amesema katika “as-Swahiyh” yake:
”al-Hassan na Mujaahid wamesema: ”Mwenye kujamiiana kwa kusahau, basi hana kitu juu yake.”[1]
Maoni ya pili yanasema kwamba mwenye kusahau ni kama mwenye kufanya kwa kukusudia na hivyo ni lazima atoe kafara na kulipa kwa kufunga, kwa sababu kujamiiana ndio kifunguzi kikubwa zaidi. Aidha ni jambo lisiloingia akili mfungaji kujamiiana kwa eti kwa kusahau. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliacha kufafanua kuhusiana aliyefanya jimaa kama alifanya hivo kwa makusudi au kwa kusahau, jambo ambalo linafahamisha kuwa hukumu ni yenye kuenea.
Maoni ya kwanza ndio yenye nguvu zaidi kutokana na nguvu ya dalili zake. Jengine ni kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwenye kufungua katika Ramadhaan kwa kusahau basi hakuna juu yake kulipa wala kafara.”[2]
[1] Tazama “Fath-ul-Baariy” (04/155-156) na “Taghliyq-ul-Ta’liyq” (03/156-157).
[2] al-Haakim (1/430).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/66-67)
- Imechapishwa: 17/03/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/66-67)
Imechapishwa: 17/03/2025
https://firqatunnajia.com/48-uliza-juu-ya-mambo-usiyoyajua-kuhusu-funga-yako/