Wanazuoni wamekhitilafiana kuhusu hukumu ya mwanamke: Je, inampasa kutoa kafara? Kuna mitazamo miwili tofauti:
1 – Hakuna kafara juu yake. Haya ndio maoni sahihi zaidi kwa Shaafi´iyyah na ndio madhehebu ya Daawuud na Ahl-udh-Dhwaahir. Aidha ni moja ya mapokezi kutoka kwa Imaam Ahmad. Ndio maoni yaliyotiwa nguvu na an-Nawawiy na Ibn Qudaamah amemili kwayo[1]. Wamesema kuwa hakuna katika Hadiyth dalili inayofahamisha kwamba kafara inamlazimu.
2 – Kafara inampasa ikiwa alikuwa radhi. Haya ni maoni Imaam Maalik, watu wa Maoni na ni mapokezi yenye nguvu zaidi kwa Imaam Ahmad na moja ya maoni ya ash-Shaafi´iy[2]. Wamesema kwamba kwa kuwa amevunja swawm ya Ramadhaan kwa kujamiiana. Hivyo basi inampasa kafara kama mwanaume. Kutajwa kwa hukumu kwa mwanaume kunahesabiwa kuwa ni hukumu kwa mwanamke pia, kwa kuwa wote wanashiriki katika uharamu wa kufungua na kuvunja heshima ya swawm.
Maonia haya ya pili ndio yenye nguvu zaidi, kwani ikiwa mwanamke alikuwa radhi katika kitendo hicho, basi analazimika kutoa kafara. Lakini ikiwa alilazimishwa, basi hana kafara juu yake. Sababu ya kutotajwa katika Hadiyth ni kwa kuwa yeye hakufika kuuliza na hali yake ilikuwa inawezekana kuwa ama alilazimishwa au alikuwa radhi. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumtaja. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ameona kwamba kafara ya mwanamke aliyelazimishwa inampasa mume wake[3]
[1] al-Umm” (03/251), “al-Muhallaa” (06/192) na “al-Mughniy” (04/375) na “al-Majmuu’” (06/339).
[2] al-Istidhkaar (10/108), “Bidaayat-ul-Mujtahid” (02/183) na “al-Mughniy” (04/375).
[3] al-Ikhtiyaaraat, uk. 109.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/67-68)
- Imechapishwa: 17/03/2025
Wanazuoni wamekhitilafiana kuhusu hukumu ya mwanamke: Je, inampasa kutoa kafara? Kuna mitazamo miwili tofauti:
1 – Hakuna kafara juu yake. Haya ndio maoni sahihi zaidi kwa Shaafi´iyyah na ndio madhehebu ya Daawuud na Ahl-udh-Dhwaahir. Aidha ni moja ya mapokezi kutoka kwa Imaam Ahmad. Ndio maoni yaliyotiwa nguvu na an-Nawawiy na Ibn Qudaamah amemili kwayo[1]. Wamesema kuwa hakuna katika Hadiyth dalili inayofahamisha kwamba kafara inamlazimu.
2 – Kafara inampasa ikiwa alikuwa radhi. Haya ni maoni Imaam Maalik, watu wa Maoni na ni mapokezi yenye nguvu zaidi kwa Imaam Ahmad na moja ya maoni ya ash-Shaafi´iy[2]. Wamesema kwamba kwa kuwa amevunja swawm ya Ramadhaan kwa kujamiiana. Hivyo basi inampasa kafara kama mwanaume. Kutajwa kwa hukumu kwa mwanaume kunahesabiwa kuwa ni hukumu kwa mwanamke pia, kwa kuwa wote wanashiriki katika uharamu wa kufungua na kuvunja heshima ya swawm.
Maonia haya ya pili ndio yenye nguvu zaidi, kwani ikiwa mwanamke alikuwa radhi katika kitendo hicho, basi analazimika kutoa kafara. Lakini ikiwa alilazimishwa, basi hana kafara juu yake. Sababu ya kutotajwa katika Hadiyth ni kwa kuwa yeye hakufika kuuliza na hali yake ilikuwa inawezekana kuwa ama alilazimishwa au alikuwa radhi. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumtaja. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ameona kwamba kafara ya mwanamke aliyelazimishwa inampasa mume wake[3]
[1] al-Umm” (03/251), “al-Muhallaa” (06/192) na “al-Mughniy” (04/375) na “al-Majmuu’” (06/339).
[2] al-Istidhkaar (10/108), “Bidaayat-ul-Mujtahid” (02/183) na “al-Mughniy” (04/375).
[3] al-Ikhtiyaaraat, uk. 109.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/67-68)
Imechapishwa: 17/03/2025
https://firqatunnajia.com/49-mwanamke-anayo-kafara-kwa-kujamiiana-na-mumewe/