48. Kumswalia maiti katika nyakati zilizokatazwa

Swali 48: Ni ipi hukumu ya kuswalia kaburi wakati uliokatazwa[1]?

Jibu: Kaburi haliswaliwi wakati wa makatazo isipokuwa ikiwa hilo limetokea katika kipindi kirefu ambacho ni baada ya swalah ya ´Aswr na swalah ya Fajr. Wakati uliokatazwa hapa ni mrefu na hivyo hapana neno kuswali ndani ya wakati huu. Kwa sababu ni miongoni mwa swalah zenye sababu. Kuhusu katika wakati ambao ni mfinyu ambao ni ule wakati uliokuja katika Hadiyh ya ´Uqbah (Radhiya Allaahu ´anh) katika “as-Swahiyh” ya Muslim ambapo amesema (Radhiya Allaahu ´anh):

“Saa tatu alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitukataza kuswali ndani yake na kuwazika ndani yake wafu wetu; wakati linapochomoza jua mpaka linaponyanyuka, jua linapolingamana sawasawa katikati ya mbingu mpaka lipinduke na jua linapokurubia kuzama mpaka lizame.”[2]

Haijuzu kumswalia maiti katika nyakati hizi na wala kumzika ndani yake kutokana na Hadiyth hii ambayo ni Swahiyh.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/156-157).

[2] Ahmad (16926) na Muslim (831).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 24/12/2021