Swali: Ni ipi hukumu ya imamu anayebeba msahafu wakati wa swalah?

Jibu: Ikiwa swalah ni ya faradhi, bora ni kutofanya hivo kutokana na kule kujishughulisha katika jambo hilo. Ikiwa swalah ni ya sunnah, kitendo hicho kinafaa. Kwa sababu swalah ya faradhi inatosha baada ya “al-Faatihah” kusoma kitu chepesi. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ

“Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan.”[1]

Lakini katika swalah ya sunnah pengine akataka kurefusha kisomo, na khaswakhaswa pale anaposwali mwenyewe au anawaswalisha watu katika Ramadhaan na akataka kukhitimisha Qur-aan pasi na kuwatia uzito watu – katika hali hiyo hakuna neno kusoma ndani ya msahafu.

[1] 73:20

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 39
  • Imechapishwa: 02/04/2022