Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ
“Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”[1]
Mwingi wa huruma ni rehema inaowapata viumbe wote.
Mwenye kurehemu ni huruma maalum kwa waumini. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا
“Naye daima ni Mwenye kuwarehemu waumini.”[2]
MAELEZO
Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu ni majina mawili miongoni mwa majina ya Allaah yanayofahamisha sifa miongoni mwa sifa Zake, nayo ni rehema. Majina yote ya Allaah (‘Azza wa Jall) yametokana na sifa yanayofahamisha maana ambazo ni sifa. Basi huchukuliwa kutoka kila jina miongoni mwa majina Yake sifa moja miongoni mwa sifa Zake.
Mwingi wa rehema ni lenye kuenea zaidi kuliko Mwenye kurehemu. Haitwi jina hilo isipokuwa Allaah pekee. Kwa maana nyingine haisemwi kwa asiyekuwa Yeye Mwingi wa rehemu.
Mwenye kurehemu hutumika kwa Allaah na kwa asiyekuwa Yeye. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Kwa hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe. Yanamuhuzunisha yale yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. Ni mpole na mwenye huruma kwa waumini.”[3]
[1] 01:02
[2] 33:43
[3] 09:128
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 53-54
- Imechapishwa: 03/06/2026
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ
“Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”[1]
Mwingi wa huruma ni rehema inaowapata viumbe wote.
Mwenye kurehemu ni huruma maalum kwa waumini. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا
“Naye daima ni Mwenye kuwarehemu waumini.”[2]
MAELEZO
Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu ni majina mawili miongoni mwa majina ya Allaah yanayofahamisha sifa miongoni mwa sifa Zake, nayo ni rehema. Majina yote ya Allaah (‘Azza wa Jall) yametokana na sifa yanayofahamisha maana ambazo ni sifa. Basi huchukuliwa kutoka kila jina miongoni mwa majina Yake sifa moja miongoni mwa sifa Zake.
Mwingi wa rehema ni lenye kuenea zaidi kuliko Mwenye kurehemu. Haitwi jina hilo isipokuwa Allaah pekee. Kwa maana nyingine haisemwi kwa asiyekuwa Yeye Mwingi wa rehemu.
Mwenye kurehemu hutumika kwa Allaah na kwa asiyekuwa Yeye. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Kwa hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe. Yanamuhuzunisha yale yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. Ni mpole na mwenye huruma kwa waumini.”[3]
[1] 01:02
[2] 33:43
[3] 09:128
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 53-54
Imechapishwa: 03/06/2026
https://firqatunnajia.com/47-mwingi-wa-rehema-jina-lisilotumika-kwa-mwengine-asiyekuwa-allaah/