47. Mtume hakumbagua anayeabudia masanamu na waja wema

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mwambie: “Umejua sasa ya kwamba Allaah kamkufurisha yule aliyeyakusudia [kuabudu] masanamu na watu wema na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akapigana nao vita?”

MAELEZO

Mwambie na umbainishie kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameonelea kuwa wale wenye kuabudu waja wema na masanamu wote ni makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipigana nao vita kwa sababu ya shirki hii na haikuwanufaisha kitu kule kuwaabudu kwao mawalii na Mitume ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 24/11/2023