47. Baadhi wanatamani dunia, wengine wanatamani Aakhirah

203 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ahmad bin al-Mufadhdhwal ametukhabarisha: Asbaatw ametukhabarisha, kutoka kwa as-Suddiy, kutoka kwa ´Abdu Khayr, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uuud, aliyesema:

“Sikuwa nafikiri kama kuna yeyote katika Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) anayetamani dunia mpaka kulipoteremshwa Aayah isemayo:

مِنكُم مَّن يُرِيدُ الدُّنْيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ الْآخِرَةَ

”Miongoni mwenu wako wenye kutaka ulimwengu na miongoni mwenu wako wenye kutaka Aakhirah.”[1]

[1] 3:152 at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” (1399).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 15/07/2025