al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
“Enyi mlioamini! Ingieni katika kujisalimisha kikamilifu na wala msifuate hatua za shaytwaan – hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.”[1]
“Abu Baswiyr ametueleza ya kwamba amemsikia Abu ´Abdillaah akisema: “Unajua ni nini kujisalimisha?” Nikasema: “Wewe ndiye mwenye kujua.” Akasema: “Uongozi wa ´Aliy, maimamu na wausiwa baada yake. Hatua za shaytwaan ni uongozi wa fulani na fulani.”
Jaabir ametueleza kwamba Abu Ja´far amesema: “Kujisalimisha ni familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah ameamrisha kujiunga nayo.”
Ja´far bin Muhammad amepokea kutoka kwa baba yake ambaye amepokea kutoka kwa baba yake ambaye amesema: “Kiongozi wa waumini amesema: “Elimu ambayo Aadam ametumwa kwayo na ambayo Mitume na Manabii wote wamefadhilishwa nayo inapatikana katika familia ya Nabii na Mtume wa mwisho.”[2]
Namna hii ndivyo Baatwiniyyah wanavyoiharibu dini ya Allaah, Kitabu Chake na Maswahabah watukufu kwa kutumia jina la familia ya Mtume. Hata hivyo familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haina lolote kuhusiana na ukafiri na uzandiki.
Namna hii Baatwiniyyah wanafadhalisha familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Mitume na Manabii wote. Ni utwevu mbaya ulioje kwa Mitume na Manabii kushinda huu? Familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si jengine isipokuwa ni waislamu katika umati wa watu. Kuna waislamu ambao ni wajuzi zaidi kuliko wao, kuna waislamu ambao ni wabora zaidi kuliko wao – seuze Mitume na Manabii.
[1] 02:208
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/102).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 79-80
- Imechapishwa: 03/04/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 79-80
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/47-al-ayyaashiy-upotoshaji-wa-kumi-na-sita-wa-al-baqarah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)