Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

76 – Imani ni moja na waumini msingi wao wanalingana katika imani hiyo. Kushindana kwa imani kati yao kunakuja katika khofu, kumcha Allaah, kuyaepuka matamanio na kulazimiana kufuata kilicho na haki zaidi.

MAELEZO

Haya ni kutokana na ile imani inayosema kuwa ni kule kukubali na kusadikisha peke yake. Hivi sasa umekwishajua kuwa imani inatofautiana katika msingi wake, na kwamba imani ya mwema inatofautiana na imani ya mtenda dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 69-70
  • Imechapishwa: 06/10/2024