Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

74 – Yale yote yaliyosihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mambo ya Shari´ah na ubainifu ni haki.

MAELEZO

Bi maana pasi na kutofautisha yale yaliyosimuliwa na msimulizi mmoja au yaliyosimuliwa na wasimulizi wengi, muda wa kuwa yamesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maoni haya ndio ya haki ambayo hapana shaka yoyote juu yake. Kutofautisha kati ya masimulizi hayo mawili ni Bid´ah na falsafa iliyopenyezwa ndani ya Uislamu na yanayotofautiana na mfumo wa Salaf na maimamu, kama nilivyothibitisha hilo katika kitabu changu kilichochapishwa na kinachotambulika ”Wujuwb-ul-Akhdh bi Hadiyth-il-Aahaad”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 69
  • Imechapishwa: 06/10/2024