45. Njia pekee ya kurekebisha jamii

Kuna wanazuoni wengine vilevile wamethibitisha msingi huu uliyothibitishwa na Shaykh-ul-Islaam. ´Allaamah na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni jambo linalotambulika kuwa Mtume wetu Muhammad (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) alianza ulinganizi wake namna hii, kuanzia Makkah kisha baadaye Madiynah. Mwisho wa Ummah huu hauwezi kutengemaa isipokuwa kwa yaleyale yaliyowafanya wa mwanzo wao kutengemaa, kama walivosema wanazuoni na waumini, miongoni mwao ni Imaam Maalik bin Anas ambaye maneno yake yalipokelewa na wanazuoni wa wakati wake na baada ya hapo. Walikubaliana naye kwamba mwisho wa Ummah huu hauwezi kutengemaa isipokuwa kwa yaleyale yaliyowafanya wa mwanzo wao kutengemaa. Kwa maana nyingine yale yaliyowafanya wale wa mwanzo kutengemaa ilikuwa kufuata Qur-aan na Sunnah, ndio kitu kipekee kitachowafanya wa mwisho wao kutengemaa mpaka siku ya Qiyaamah. Yeyote anayetaka kurekebisha jamii ya Kiislamu, au anataka kurekebisha jamii nyingine katika dunia hii, kwa mifumo na njia zingine kuliko zile zilizowatengeneza wale wa mwanzo, basi amekosea na amezungumza isiyokuwa haki. Hakuna kingine kinachowezekana kisichokuwa hiki. Hakika si venginevyo njia pekee ya kuwatengeneza watu na kuwafanya wakasimama katika njia ilionyooka, ni ile njia ambayo alipita juu yake Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakapita juu yake Maswahabah zake watukufu (Radhiya Allaahu ´anhum) na baadaye wale waliowafuata kwa wema mpaka hii leo.”[1]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (1/249).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 62
  • Imechapishwa: 23/05/2023