Ahl-ul-Hadiyth wanaharamisha ulevi uliyotengenezwa na zabibu, tende, asali, mahindi au kitu kingine kinacholevya. Wanaharamisha kiwango chake kidogo na kiwango chake kikubwa. Wanajiepusha nayo, wanaizingatiwa kuwa ni najisi na wanaona adhabu juu yake.

Wanaona kufanya haraka kutekeleza swalah. Kwa ajili ya kutaraji kupata thawabu nzuri wanaona bora ni kuiswali mwanzoni mwa wakati kuliko kuichelewesha mwishoni mwa wakati wake.

Wanaona kuwa ni wajibu kusoma al-Faatihah nyuma ya imamu.

Wanaamrisha kukamilisha Rukuu´ na Sujuud na kuzingatia ukamilishwaji wake kuwa ni jambo la wajibu. Wanaona kuwa kukamilisha Rukuu´ na Sujuud kwa kutulia, kuinuka kutoka katika Rukuu´, kunyooka sawasawa na kutulia wakati wa kuinuka kutoka kwenye Rukuu´ na pia kutulia wakati wa kutoka kwenye Sujuud na kukaa kati ya Sujuud mbili hali ya utulivu kwamba ni katika nguzo za swalah. Swalah haisihi isipokuwa kwa mambo hayo.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 297-298
  • Imechapishwa: 26/12/2023