Wanaamini kuwa Allaah (Subhaanah) amewaumba mashaytwaan; wanawatia wasiwasi wanadamu, wanakusudia kuwapotosha na kuwadanganya. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ

”Hakika mashaytwaan wanadokeza marafiki wao wa ndani ili wabishane nanyi. Na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.”[1]

Allaah (Ta´ala) anawatawalisha kwa yule Anayemtaka na anamlinda dhidi ya vitimbi na njama zao Anayemtaka. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ وَعِدْهُمْ ۚ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ ۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلًا

”Wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako na wakusanyie kikosi chako cha farasi, na askari wako waendao kwa miguu, na shirikiana nao katika mali na watoto na waahidi, lakini shaytwaan hawapi ahadi isipokuwa ni udanganyifu. Hakika waja Wangu huna mamlaka juu yao, na Mola wako anatosheleza kuwa mtegemewa wa yote.”[2]

إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ

“Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na kwa Mola wao wanategemea. Hakika mamlaka yake ni juu ya wale wanaomfanya rafiki na ambao wao wanamshirikisha [Allaah] naye.”[3]

[1] 6:121

[2] 17:64-65

[3] 16:99-100

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 296
  • Imechapishwa: 26/12/2023