Swali : Je, inafaa kukata miti inayoudhi makaburini?

Jibu: Inatakiwa kuikata. Kwa sababu inawaudhi wenye kuja kuyatembelea na khaswa ile yenye miiba. Lakini ikiwa baadhi ya wajinga wanaitakidi kuwa na baraka kwa sababu kwa madai yao wanaona kuwa inaota juu ya kaburi la walii, miti hii ni lazima kuikata kabisa. Kufanya hivo kunaondosha njia zinazopelekea katika shirki na kuchupa mpaka kwa wafu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 139-140
  • Imechapishwa: 25/07/2022