Swali: Ni ipi hukumu ya kuadhini na kukimu kwenye kaburi la maiti wakati anapowekwa ndani?

Jibu: Hapana shaka kwamba jambo hilo ni Bid´ah ambayo Allaah hakuiteremshia hoja yoyote. Kwa sababu jambo hilo halikunakiliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Kheri zote zinapatikana kwa kuwafata wao na kwa kufuata njia yao. Amesema (Subhaanah):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Wale waliotangulia mwanzoni ambao ni Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua kitendo kisichokuwa katika amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika tamko jengine:

 “Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[3]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa na kila Bid´ah ni upotevu.”[4]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kutoka katika Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh).

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

[1] 09:100

[2] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).

[3] Muslim (1718).

[4] Muslim (867).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 25/07/2022