Maneno yake mtunzi:

“Anazungumza kwa maneno ya milele… “

Aina ya maneno yake ni milele na yanazuka kutegemea na matukio ndio maana pekee inayoendana na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ingawa udhahiri wa maneno yake aina yake ni ya milele na yenye kuzuka.

Maneno yake mtunzi:

”Muusa (´alayhis-Salaam) aliyasikia kutoka Kwake pasi na mkati kati.”

Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ

“Nami nimekuchagua, basi sikiliza yanayofunuliwa Wahy.”[1]

Maneno yake mtunzi:

”Vilevile Jibiriy (´alayhis-Salaam) aliyasikia… “

Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِنْ رَبِّكَ

“Sema: ”Roho takatifu ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki.”[2]

Maneno yake mtunzi:

“… vivyo hivyo Malaika wengine aliyowaidhinisha na Mitume Yake.”

Kuhusu Malaika ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mola wetu anapohukumu amri ya jambo fulani basi husabihi wabebaji wa ´Arshi, kisha wakasabihi wakazi wa mbingu inayofuata mpaka Tasbiyh inawafikia wakazi wa mbingu ya chini. Wale wakazi walioko chini ya wabebaji wa ´Arshi huwauliza wabebaji wa ´Arshi:

مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ

“Amesema nini Mola wenu?”[3]

ambapo wakawaeleza.”

Ameipokea Muslim[4].

Kuhusu Mitume imethibiti kuwa Allaah amemzungumzisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa kupandishwa mbinguni[5].

Maneno yake mtunzi:

“Hakika Yeye (Subhaanah) atawazungumzisha waumini Aakhirah na [wao waumini] watazungumza Naye… “

Abu Sa´iyd al-Khudriy ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah atawaambia watu wa Peponi: “Enyi watu wa Peponi!” Watasema: “Tunakuitikia, Mola wetu, na nakuomba msaada.””[6]

Kuna maafikiano juu yake.

Maneno yake mtunzi:

”Atawapa idhini wamtembelee.”

Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika watu wa Peponi watapoingia ndani basi watashushwa kutokana na fadhilah za matendo yao kisha atawapa idhini kwa kiwango cha siku ya ijumaa katika masiku ya dunia ambapo wamtembelee Mola wao… “

Ameipokea Ibn Maajah na at-Tirmidhiy ambaye amesema: “Ni geni.” Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy[7].

Maneno yake mtunzi:

´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Allaah anapotamka kwa Wahy, sauti Yake wanaisikia walioko mbinguni.”

Hilo limepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Sikupata Athar ya Ibn Mas´uud kwa muundo huu. Ibn Khuzaymah ametaja njia zake katika “Kitaab-ut-Tawhiyd” kwa matamshi mbalimbali ikiwa ni pamoja na tamko lisemalo:

“Allaah anapozungumza kwa Wahy, wakazi wa mbinguni husikia sauti Yake kama vile mnyororo juu ya mlima na hushuka chini wakasujudu.”

Kuhusu mpokeaji kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kutoka katika Hadiyth ya an-Nawwaas bin Sam´aan aliyeeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapotaka kufunua amri ya jambo fulani basi Huzungumza kwa Wahy. Hapo ndipo mbingu hutetemeka sana – au alisema radi kali – kwa sababu ya kumuogopa Allaah. Wanapoyasikia hayo wakazi wa mbinguni basi huanguka chini hali ya kusujudu… “[8]

Ameipokea Ibn Khuzaymah na Ibn Abiy Haatim.

[1] 20:13

[2] 16:102

[3] 34:23

[4] Muslim (2229).

[5] al-Bukhaariy (3887) na Muslim (164).

[6] al-Bukhaariy (6530) na Muslim (222).

[7] Hadiyth dhaifu. Ni sehemu ya Hadiyth ndefu aliyoipokea al-Tirmidhiy (2552) na Ibn Maajah (4336). Katika cheni ya wapokezi wake yuko ´Abdul-Humayd bin Habiyb bin Abiy-´Ishriyn ambaye ni mtunzi wa al-awzaa´iy. Amesema mtunzi wa ”at-Taqriyb”, uk. 333:

”Ni mkweli na wakati mwingine hukosea.”

Abu Haatim amesema:

”Alikuwa mwandishi lakini hakuwa msomi wa Hadiyth. Kwa ajili hiyo ndio maana at-Tirmidhiy amemdhoofisha kwa kusema:

”Hadiyth ni geni.”

Akimaanisha kuwa ni dhaifu.

[8] at-Twabaraaniy katika ”Musnad-ush-Shaamiyyiyn” (591).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 74-76
  • Imechapishwa: 31/10/2022