Katika mambo yanayokatazwa kwa mfungaji ni kupitiliza katika kusukutua mdomo na kuvuta maji puani. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Fanya kishindo katika kupalizia isipokuwa kama utakuwa umefunga.”[1]
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Hilo ni kwa sababu mtu anapovuta maji kwa nguvu kupitia pua, maji hushuka mpaka kooni na tumboni na hapo humpata yaliyo sawa na anayekunywa kwa mdomo wake. Mwili wake hunufaika na maji hayo kama anavyonufaika kwa kunywa na kiu huondoka kwa kunywa maji.”
[1] Abu Daawuud (142) na (143), Ibn Maajah (407), Ibn Khuzaymah (150), Ibn Hibbaan (159), al-Haakim (01/147-148), Ahmad (04/33). Ni Swahiyh kwa mujibu wa adh-Dhahabiy na Ibn Hazm.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 43
- Imechapishwa: 15/03/2026
Katika mambo yanayokatazwa kwa mfungaji ni kupitiliza katika kusukutua mdomo na kuvuta maji puani. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Fanya kishindo katika kupalizia isipokuwa kama utakuwa umefunga.”[1]
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Hilo ni kwa sababu mtu anapovuta maji kwa nguvu kupitia pua, maji hushuka mpaka kooni na tumboni na hapo humpata yaliyo sawa na anayekunywa kwa mdomo wake. Mwili wake hunufaika na maji hayo kama anavyonufaika kwa kunywa na kiu huondoka kwa kunywa maji.”
[1] Abu Daawuud (142) na (143), Ibn Maajah (407), Ibn Khuzaymah (150), Ibn Hibbaan (159), al-Haakim (01/147-148), Ahmad (04/33). Ni Swahiyh kwa mujibu wa adh-Dhahabiy na Ibn Hazm.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 43
Imechapishwa: 15/03/2026
https://firqatunnajia.com/44-mfungaji-ajiepushe-kusukutua-na-kupatiliza-kwa-kishindo/