5 – Maoni ya Imaam Ibn Rushd al-Maalikiy:
”Wametofautiana kuhusu kupangusa juu ya soksi. Sababu ya kutofautiana kwao ni kutofautiana kwao katika usahihi wa Hadiyth zilizopokewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alipangusa juu ya soksi na viatu. Vilevile tofauti yao inatokana na kwamba mtu anaweza kulinganisha kitu kingine na soksi za ngozi au ni ´ibaadah isiyolinganishwa wala isiyovukwa mipaka yake. Basi yule ambaye ameona kuwa Hadiyth haikusihi, haikumfikia na hakuona kuwa inafaa kuzilinganisha na soksi za ngozi, ameona kuwa inafaa tu kupangusa juu yake. Na yule ambaye Hadiyth zimesihi kwake na akaona kufaa kuzilinganisha na soksi za ngozi, ameona kuwa inafaa kupangusa juu ya soksi za kawaida.”
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 68
- Imechapishwa: 16/04/2026
5 – Maoni ya Imaam Ibn Rushd al-Maalikiy:
”Wametofautiana kuhusu kupangusa juu ya soksi. Sababu ya kutofautiana kwao ni kutofautiana kwao katika usahihi wa Hadiyth zilizopokewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alipangusa juu ya soksi na viatu. Vilevile tofauti yao inatokana na kwamba mtu anaweza kulinganisha kitu kingine na soksi za ngozi au ni ´ibaadah isiyolinganishwa wala isiyovukwa mipaka yake. Basi yule ambaye ameona kuwa Hadiyth haikusihi, haikumfikia na hakuona kuwa inafaa kuzilinganisha na soksi za ngozi, ameona kuwa inafaa tu kupangusa juu yake. Na yule ambaye Hadiyth zimesihi kwake na akaona kufaa kuzilinganisha na soksi za ngozi, ameona kuwa inafaa kupangusa juu ya soksi za kawaida.”
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 68
Imechapishwa: 16/04/2026
https://firqatunnajia.com/43-maoni-ya-ibn-rush-kuhusu-kupangusa-juu-ya-soksi/