Desturi ya Ibn Rushd katika kitabu chake kilichotajwa ni kufafanua misingi ya wanazuoni wanaofanya ijtihadi, isipokuwa kila suala ambalo misingi yake imekuwa mingi na maneno yakatawanyika juu yake, basi haki iko katika moja yake bila shaka, nayo ni ile ambayo dalili yake imesihi na msingi wake ukawa na nguvu. Dalili imesihi hapa katika kupaka juu ya soksi na msingi wake umeimarika kwa yale tuliyoyanukuu kabla na tutakayonukuu baadaye. Ndiyo maana Imaam an-Nawawiy amesema wakati alipokuwa akimraddi Imaam Maalik maoni yake ambaye anaona kuwa inachukiza kufunga siku sita za Shawwaal:
”Ikithibiti Sunnah haiachwi kwa sababu ya kuachwa na baadhi ya watu, wengi wao au wote wao.”
Hivyo ndivyo inavyosemwa katika kupaka juu ya soksi: haiachiwi baada ya kuthibiti kwake kwa sababu ya tofauti ya anayepinga au kwa kipimo cha anayepima. Kwa sababu hakuna ijtihadi mbele ya andiko la Qur-aan na Sunnah. Tunajitakasa kwa Allaah kutokana na kuyakataa Maandiko kwa vipimo na maono.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 68-69
- Imechapishwa: 16/04/2026
Desturi ya Ibn Rushd katika kitabu chake kilichotajwa ni kufafanua misingi ya wanazuoni wanaofanya ijtihadi, isipokuwa kila suala ambalo misingi yake imekuwa mingi na maneno yakatawanyika juu yake, basi haki iko katika moja yake bila shaka, nayo ni ile ambayo dalili yake imesihi na msingi wake ukawa na nguvu. Dalili imesihi hapa katika kupaka juu ya soksi na msingi wake umeimarika kwa yale tuliyoyanukuu kabla na tutakayonukuu baadaye. Ndiyo maana Imaam an-Nawawiy amesema wakati alipokuwa akimraddi Imaam Maalik maoni yake ambaye anaona kuwa inachukiza kufunga siku sita za Shawwaal:
”Ikithibiti Sunnah haiachwi kwa sababu ya kuachwa na baadhi ya watu, wengi wao au wote wao.”
Hivyo ndivyo inavyosemwa katika kupaka juu ya soksi: haiachiwi baada ya kuthibiti kwake kwa sababu ya tofauti ya anayepinga au kwa kipimo cha anayepima. Kwa sababu hakuna ijtihadi mbele ya andiko la Qur-aan na Sunnah. Tunajitakasa kwa Allaah kutokana na kuyakataa Maandiko kwa vipimo na maono.
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 68-69
Imechapishwa: 16/04/2026
https://firqatunnajia.com/44-wakati-sunnah-inapothibiti-hakuna-maoni-ya-yeyote/