Kuingia msikiti Mtukufu kwa viatu

Swali: Ni ipi hukumu ya wanaotembelea kwa viatu vyao katika msikiti Mtukufu?

Jibu: Ni jambo lisilotakikana kwa sababu kitendo hicho kinawafungulia mlango wale wasiokuwa na elimu ambao hawautukuzi msikiti Mtukufu, hivyo wakaanza kuingia na viatu vilivyo na maji, na pengine hata vikawa na uchafu.  Ikiwa jambo linalotakikana kwa mujibu wa Shari´ah kunachelea juu yake kupelekea katika madhara zaidi kuliko manufaa, basi itakuwa ni wajibu kuzingatia madhara hayo na kuliacha. Kanuni inasema kwamba pindi yanapokutana manufaa na madhara, basi ni wajibu kuzingatia yale madhara na kuyaacha yale manufaa. Mtume alitaka kuibomoa Ka´bah na kujenga upya misingi yake kutokana na misingi ya Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam), lakini kwa vile watu ndio punde walikuwa wamesimuli akaachana na jambo hilo kwa kuchelea madhara. Alimwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Ee ´Aaishah! Kama isingelikuwa watu wako ndio punde wametoka kusilimu basi ningeibomoa Ka´bah, nikaijenga kutokana na misingi ya Ibraahiym na kuifanya kuwa na milango miwili; mlango ambao watu wanaingilia na mlango wanaotokea.”[1]

[1] al-Bukhaariy (126).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/386-387)
  • Imechapishwa: 16/04/2026