Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na viatu? Kuwepo kwa mikeka hii leo kwenye misikiti kunawazuilia watu kuswali na viatu?
Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah. al-Bukhaariy na Muslim wote wawili wamepokea kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali na viatu. Isitoshe Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jitofautisheni na mayahudi kwani hakika wao hawaswali kwa soksi zao za ngozi wala viatu vyao.”[1]
Mazulia hayamzuilii mtu kuswali na viatu. Hata hivyo jambo ambalo watu wengi wanaghafilika nalo ni kutazama kwao viatu vyao kabla ya kuingia msikitini, jambo ambalo linakwenda kinyume na yale aliyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapokuja mmoja wenu msikitini, basi atazame kwanza. Akiona uchafu au taka kwenye viatu vyake, basi avipanguse na aswali ndani yake.”[2]
Watu wangelitendea kazi Hadiyth hii, basi kusingelikuwa na madhara endapo watu wataswali ndani ya viatu vyao.
[1] Abu Daawuud (652) na Ibn Hibbaan (3186).
[2] Ahmad (3/20) na Abu Daawuud (650).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/387-388)
- Imechapishwa: 16/04/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na viatu? Kuwepo kwa mikeka hii leo kwenye misikiti kunawazuilia watu kuswali na viatu?
Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah. al-Bukhaariy na Muslim wote wawili wamepokea kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali na viatu. Isitoshe Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jitofautisheni na mayahudi kwani hakika wao hawaswali kwa soksi zao za ngozi wala viatu vyao.”[1]
Mazulia hayamzuilii mtu kuswali na viatu. Hata hivyo jambo ambalo watu wengi wanaghafilika nalo ni kutazama kwao viatu vyao kabla ya kuingia msikitini, jambo ambalo linakwenda kinyume na yale aliyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapokuja mmoja wenu msikitini, basi atazame kwanza. Akiona uchafu au taka kwenye viatu vyake, basi avipanguse na aswali ndani yake.”[2]
Watu wangelitendea kazi Hadiyth hii, basi kusingelikuwa na madhara endapo watu wataswali ndani ya viatu vyao.
[1] Abu Daawuud (652) na Ibn Hibbaan (3186).
[2] Ahmad (3/20) na Abu Daawuud (650).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/387-388)
Imechapishwa: 16/04/2026
https://firqatunnajia.com/tazama-viatu-vyako-kwanza/