Wanaitakidi na kushuhudia ya kwamba Allaah (´Azza wa Jall) amemuwekea kila kiumbe muda wake wa kueshi na kwamba hakuna nafsi yoyote itayokufa isipokuwa kwa idhini ya Allaah na kwa wakati maalum iliyowekewa. Unapofika wakati wa mtu wa kufa basi hakuna namna yoyote ya kuuepuka. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ
”Na kila ummah una muda waliowekewa, basi utakapofika muda wao huo, hawatocheleweshwa wala hawatatangulia.”[1]
وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ كِتَابًا مُّؤَجَّلًا
”Na haiwezekani nafsi yeyote kufa isipokuwa kwa idhini ya Allaah, kwani imeandikiwa muda wake maalum.”[2]
Wanashuhudia ya kwamba ambaye anakufa au kuuliwa basi umemalizika muda wake. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ
“Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia wafe.”[3]
Amesema tena (Ta´ala):
أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ
“Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika ngome zilizo na nguvu.”[4]
[1] 7:34
[2] 3:145
[3] 3:154
[4] 4:78
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)