43. Ahl-us-Sunnah hawaendi kombo kutokana na yale yaliyokuja kutoka kwa Mitume

Kwa sababu hiyo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Kumuamini Allaah ina maana ni pamoja na kuamini yale aliyojisifia Mwenyewe katika Kitabu Chake na kwa yale aliyomsifia kwayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bila ya upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kufananisha. Bali wao wanaamini yafuatayo kuhusiana na Allaah (Subhaanah):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]

Hawakanushi kutoka Kwake yale ambayo amejisifu Mwenyewe na wala hawapotoshi maana ya maneno kuyatoa mahala pake. Hawaharibu majina ya Allaah na Aayah Zake. Hawaainishi maana Yake halisi, hawazifananishi na kuzilinganisha sifa Zake na sifa za viumbe Wake. Hakika Yeye (Subhaanah) hana mshirika wala mwenza na wala halinganishwi na viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwani, hakika Yeye (Subhaanah) ni Mjuzi zaidi wa kujijua Mwenyewe na wengine na ni Mkweli zaidi kwa Kauli na Maneno yaliyo bora na ya wazi kuliko Viumbe Vyake. Halafu Mitume Wake ni wakweli na ni wenye kusadikishwa, tofauti na wale wanaosema juu Yake yale wasioyajua. Na kwa ajili ya hii ndio maana amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Ametakasika Mola wako Mola Mtukufu kutokana na yote wanayoelezea na amani iwe juu ya Mitume na himidi zote ni za, Mola wa walimwengu.”[2]

Hivyo kaelezea kuitakasa nafsi Yake Mwenyewe kwa waliyomuelezea wale waendao kinyume na Mitume, akawaswalia Mitume Wake kuonyesha dalili ya usalama wa waliyoyasema katika mapungufu na kasoro.

Na Yeye (Subhaanah) kwa yale aliyojisifia na kujiita kwayo Mwenyewe, kajumuisha baina ya ukanushaji na uthibitisho. Hivyo Ahl-usSunnah wal-Jamaa´ah hawaendi kombo kutokana na hawaendi kombo kutokana na yale waliyokuja nayo Mitume, kwani hakika ni Njia iliyonyooka; Njia ambayo Kawaneemesha Kwayo waifuatayo, miongoni mwa Manabii, wakweli, mashahidi na waja wema.”[3]

[1] 42:11

[2] 37:181-182

[3] al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 49.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 05/12/2025