42. Matahadharisho ya kutokuwa mlinganizi wa upotevu

Muislamu atahadhari asiwe katika walinganizi wa upotevu. Si kwamba atapata madhambi yeye peke yake. Bali atabeba madhambi pia ya wale watakaomfuata. Kwa kuwa yeye ndiye kawaghuri, kuwahadaa na akawafungulia mlango wa shari. Hivyo akawa ni kiigizo katika shari. Amesema (Ta´ala):

لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ

“Ili wabebe madhambi yao kamili siku ya Qiyaamah na madhambi ya wale waliowapoteza bila ya elimu. Tanabahi!  Uovu ulioje wanayoyabeba!” (16:25)

Kuna khatari kubwa juu ya hili. Hili linazidi kuwa ni msisitizo kwa muislamu ya kwamba anatakiwa awe ni kiigizo katika kheri na alinganie katika kheri. Ajiepushe asiwe ni mlinganizi katika shari, kufuata matamanio au mikhalafa. Haijalishi kitu ni nani ambaye yuko katika hayo. Hakika haki ina haki zaidi ya kufuatwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 107
  • Imechapishwa: 10/01/2024