41. Jahmiyyah, Mu´tazilah na vifaranga vyao wamekula khasara

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

روى ذاك قومٌ لا يردُّ حديثُهم

14 – Wameyapokea hayo watu zisizorudishwa Hadiyth zao

ألا خابَ قومٌ كذبوهم وقُبِّحوا

     Tanabahini! Wamekula khasara watu waliowakadhibisha na wabezwe

MAELEZO

Wamepokea Hadiyth kuhusu Kushuka kundi kubwa la Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“… zisizorudishwa Hadiyth zao.”

Kwa sababu ni Hadiyth zilizopokewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jahmiyyah na wakanushaji hawana njia yoyote inapokuja katika cheni ya wasimulizi.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tanabahini! Wamekula khaara watu… “

Kwa kuwa wamekadhibisha Hadiyth hizi na wakapinga kuwa Allaah anashuka na wakapindisha maana ya Hadiyth za Mtume kinyume na alivyokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wamemzulia na kumsemea uwongo Allaah.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“… waliowakadhibisha na wabezwe.”

Nao ni Jahmiyyah na wale wenye kufuata mfumo wao. Msingi wa balaa ni Jahmiyyah na Mu´tazilah. Wote waliokuja baada yao wakafuata ´Aqiydah hiyo. Wao ndio ambao wamefungua mlango wa upotevu. Wapotevu wote waliokuja baada yao ni wenye kuwafuata. Wanaguswa na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuita katika upotevu atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya ambaye atamfuata, hakutopungua kitu katika madhambi yao, na mwenye kulingania katika uongofu atakuwa na ujira mfano wa ujira wa ambaye atamfuata, hakutopungua kitu katika ujira wao.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7321) na Muslim (16) na (2674)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 106
  • Imechapishwa: 10/01/2024