2- Hali kadhalika kutawassul kwa du´aa za watu wema waliohai. Ni jambo linalofaa.  Kama jinsi ´Umar alivyotawassul kwa ´Abbaas na akamuomba du´aa na Mu´aawiyah akatawassul kwa du´aa ya Yaziyd al-Jarshiy. Kwa ajili hii wanachuoni wamesema katika “Kitaab-ul-Istisqaa´”:

“Imependekezwa kutawassul kwa waja wema.”[1]

Kama alivyofanya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh). Makusudio sio kutawassul kwa haki zao, nafasi zao na jaha zao.

Kutawassul kwa jaha au kwa haki ya mtu na nafasi ya mtu mbele ya Allaah, hizi ni Tawassul zilizozuliwa na kuharamishwa. Vilevile ni njia katika njia zinazopelekea katika shirki.

[1] Tazama “al-Mughniy” (3/346) na “al-Kaafiy” (1/535).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 69
  • Imechapishwa: 11/08/2018