185 – Nimesoma kitabu ambacho Abu Sa´iyd Muhammad bin Muusa as-Swayrafiy ametutajia ya kwamba amekisikia kutoka kwa Abul-´Abbaas Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ambapo al-´Atiyqiy akanikhabarisha kwa njia ya kunisomea nacho: ´Uthmaan bin Muhammad al-Mukharramiy ametukhabarisha: al-Aswamm amenikhabarisha kwamba al-´Abbaas bin Muhammad ad-Duuriy amewadithia: ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuzindua, kutoka kwa Sa´iyd bin Saalim, ambaye amesema:

”Siku moja ya kiangazi Rawh bin Zinbaa´ alitua baina ya Makkah na Madiynah. Aliandaa chakula chake cha jioni ambapo mchungaji akaanguka kutoka mlimani. Akasema: ”Ee mchungaji, njoo kwenye chakula cha jioni!” Akasema: ”Mimi nimefunga.” Rawh akasema: ”Unafunga katika joto hili kali?” Mchungaji yule akasema: ”Niyaache masiku yangu kwenda kupita bure namna hii?” Ndipo Rawh akasoma:

Unayachunga masiku hayo, ee mchungaji

wakati Rawh bin Zinbaa´anayapoteza

186 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Abu Ja´far ´Abdullaah bin Ismaa´iyl bin Ibraahiym al-Haashimiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Ubayd al-Qurashiy ametuhadithia: Baadhi ya wanazuoni wamenihadithia:

”Siku moja ambapo kulikuwa na joto kali kundi la watu lilimwalika bwana mmoja kwenye chakula. Bwana yule akasema: ”Mimi nimefunga.” Wakasema: ”Katika siku kama hii?” Akasema: ”Kwa hiyo niyapoteze masiku yangu?”

187 – ´Aliy bin Muhammad al-Mu-addil amenikhabarisha: al-Husayn bin Swafwaan ametuzindua: Abu Bakr bin Abiyd-Dunyaa ametuhadithia: Baadhi ya wanazuoni wamenihadithia:

”Kundi la watu lilimwalika bwana mmoja katika chakula. Bwana yule akasema: ”Mimi nimefunga.” Wakasema: ”Fungua na ufunge kesho.” Ndipo akasema: ”Ni nani anayenipa dhamana ya kesho?”

188 – Abul-Fath Muhammad bin Ahmad bin Abiyl-Fawaaris al-Haafidhw ametukhabarisha: ´Aliy bin ´Abdillaah bin al-Mughiyrah ametukhabarisha: Ahmad bin Sa´iyd ad-Dimashqiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin al-Mu´tazz amesema:

”Tumia fursa zinazowezekana na wala usisubiri kesho. Ni nani awezaye kukudhamini kesho?”

189 – Abul-Qaasim al-Azhariy ametukhabarisha: Sahl bin Ahmad ad-Diybaajiy ametuzindua: Muhammad bin Muhammad bin al-Ash´ath al-Kuufiy ametuhadithia Misri: Muusa bin Ismaa´iyl bin Muusa bin Ja´far bin Muhammad ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake ´Aliy bin al-Husayn, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa ´Aliy amesema:

”Fanya matendo ya kila siku na hivyo utaongozwa.”

190 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Muhammad bin Muhammad bin Ahmad bin Maalik al-Iskaafiy ametuzindua: Abul-Ahwas Muhammad bin al-Haytham al-Qaadhwiy ametuhadithia: Muhammad bin Kathiyr ametuhadithia, kutoka kwa Makhlad bin Husayn, kutoka kwa Hishaam: Hafswah bint Siyriyn alikuwa akisema:

”Enyi vijana, fanyeni matendo! Hakika matendo yanafanywa katika ujana.”

191 – ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Muqri’ al-Hadhdhwaa’ amenikhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bazzaaz amenikhabarisha: Muhammad bin Ahmad bin Haaruun al-Faqiyh ametuhadithia: Ibraahiym bin ´Abdillaah bin al-Junayd amenihadithia: Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: ´Ubaydullaah bin Muhammad bin Hafsw al-Qurashiy ametuhadithia, kutoka kwa baba yake: Mtu mmoja katika wenye hekima alimwandikia mmoja katika ndugu zake vijana:

”Hakika nimeona wengi wanaokufa ni vijana. Linajulisha kuwa wazee ni wachache.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 104-107
  • Imechapishwa: 27/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy