al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga mfano wa bakhili na mwenye kutoa swadaqah kama watu wawili waliovaa koti mbili za chuma ambazo zimebana mikono yao hadi kwenye vifua na koo zao. Hivyo ikawa mwenye kutoa swadaqah kila anapotoa swadaqah, basi koti la yule mtoaji lilikuwa likipanuka mpaka kufika kwenye vidole vyake na kufuta athari yake. Ikawa yule bakhili kila alipotamani kutoa swadaqah, koti lake la chuma lilizidi kubana na kila pete ya chuma hukaa mahali pake, haipanuki.” Mimi nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya kwa kidole chake katika koti lake, nilimuona analipanua lakini halipanuki.”[1]
Wakati ilipokuwa kwamba bakhili anazuiliwa kutoa wema, ananyimwa fadhilah na kheri, basi malipo yake ikawa ni kwa mujibu wa matendo yake. Ana moyo uliofinyangwa, hana faraja, ni mwenye kifua kidogo, nafsi dhaifu, furaha chache na ni mwenye huzuni nyingi na mashaka. Hajawahi kukamilishiwa haja wala kusaidiwa katika kile anakihitaji. Hali yake ni kama ya mtu aliyevaa koti la chuma mikono yake imefungwa hadi shingoni, kwa namna ya kwamba hawezi kuitoa wala kuihamisha. Kila alipotamani kuitoa au kupanua koti hiyo, basi kila pete ya chuma hukaa mahali pake. Ndivyo ilivyo kwa bakhili; kila anapotamani kutoa swadaqah basi ubakhili wake humzuia na moyo wake hubaki kifungoni kama ulivyo. Mtoaji wa swadaqah kila anapotoa swadaqah basi moyo wake hufunguka, kifua chake hupana. Ni kama upanuzi wa koti hilo juu yake. Kila anapotoa swadaqah, basi moyo wake hupana zaidi, furaha yake huongezeka na bashasha yake huwa kubwa. Lau hakuna faida nyingine katika swadaqah isipokuwa hii tu, basi ingemstahiki mja awe mwenye kujiongezea katika swadaqah na mwenye kuharakisha kuitoa. Allaah amesema:
وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
”Yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (5797) na Muslim (1021).
[2] 59:9 na 64:16
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 73-75
- Imechapishwa: 11/08/2025
al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga mfano wa bakhili na mwenye kutoa swadaqah kama watu wawili waliovaa koti mbili za chuma ambazo zimebana mikono yao hadi kwenye vifua na koo zao. Hivyo ikawa mwenye kutoa swadaqah kila anapotoa swadaqah, basi koti la yule mtoaji lilikuwa likipanuka mpaka kufika kwenye vidole vyake na kufuta athari yake. Ikawa yule bakhili kila alipotamani kutoa swadaqah, koti lake la chuma lilizidi kubana na kila pete ya chuma hukaa mahali pake, haipanuki.” Mimi nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya kwa kidole chake katika koti lake, nilimuona analipanua lakini halipanuki.”[1]
Wakati ilipokuwa kwamba bakhili anazuiliwa kutoa wema, ananyimwa fadhilah na kheri, basi malipo yake ikawa ni kwa mujibu wa matendo yake. Ana moyo uliofinyangwa, hana faraja, ni mwenye kifua kidogo, nafsi dhaifu, furaha chache na ni mwenye huzuni nyingi na mashaka. Hajawahi kukamilishiwa haja wala kusaidiwa katika kile anakihitaji. Hali yake ni kama ya mtu aliyevaa koti la chuma mikono yake imefungwa hadi shingoni, kwa namna ya kwamba hawezi kuitoa wala kuihamisha. Kila alipotamani kuitoa au kupanua koti hiyo, basi kila pete ya chuma hukaa mahali pake. Ndivyo ilivyo kwa bakhili; kila anapotamani kutoa swadaqah basi ubakhili wake humzuia na moyo wake hubaki kifungoni kama ulivyo. Mtoaji wa swadaqah kila anapotoa swadaqah basi moyo wake hufunguka, kifua chake hupana. Ni kama upanuzi wa koti hilo juu yake. Kila anapotoa swadaqah, basi moyo wake hupana zaidi, furaha yake huongezeka na bashasha yake huwa kubwa. Lau hakuna faida nyingine katika swadaqah isipokuwa hii tu, basi ingemstahiki mja awe mwenye kujiongezea katika swadaqah na mwenye kuharakisha kuitoa. Allaah amesema:
وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
”Yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (5797) na Muslim (1021).
[2] 59:9 na 64:16
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 73-75
Imechapishwa: 11/08/2025
https://firqatunnajia.com/41-mfano-wa-mbakhili-na-mtoa-swadaqah/