Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amempigia mfano mtoa swadaqah na mtu aliyeletwa akatwe shingo ambapo akajikomboa kwa mali yake kwa kiwango cha kutosha. Hakika swadaqah humkomboa mja kutokana na adhabu ya Allaah (Ta´ala). Kwa sababu dhambi na makosa yake yanamlazimu kuangamia, lakini swadaqah huja na kumkomboa kutoka katika adhabu hiyo na kumfungua kwayo. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh alipowakhutubia wanawake siku ya ‘Iyd:
“Enyi wanawake, toeni swadaqah japo kwa sehemu ya mapambo yenu. Kwani nimewaona kuwa nyinyi ni wengi zaidi miongoni mwa watu wa Motoni.”[1]
´Adiy bin Haatim ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa Mola wake atamzungumzisha na hakutokuwepo mkalimani yeyote baina yao. Atatazama upande wa kulia wake na hataona isipokuwa yale aliyoyatanguliza, atatazama upande wa kushoto wake na hataona isipokuwa aliyoyatanguliza, atatazama mbele yake na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Hivyo basi uogopeni Moto, japo kwa nusu ya tende.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
“Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Ni kitu gani kitamwokoa mja kutoka Motoni?” Akasema: “Kumwamini Allaah.” Nikamuuliza: “Ee Nabii wa Allaah, pamoja na imani kuna kitendo gani?” Akasema: “Utoe katika yale aliyokupa Allaah au utoe katika yale aliyokuruzuku Allaah.” Nikamuuliza: “Ee Nabii wa Allaah, ikiwa ni masikini asiyepata cha kutoa?” Akasema: “Aamrishe mema na kukataza maovu.” Nikamuuliza: “Vipi Akiwa hawezi kuamrisha mema na kukataza maovu?” Akasema: “Basi amsaidie asiyejua.” Nikamuuliza: “Ewe Mtume wa Allaah, vipi kama hajui kutenda chochote?” Akasema: “Basi amsaidie aliyedhulumiwa.” Nikamuuliza: “Ee Mtume wa Allaah, vipi ikiwa ni dhaifu hawezi kumsaidia aliyedhulumiwa?” Akasema: “Unataka kumuachia nini rafiki yako katika wema? Azuie madhara yake kwa watu.” Nikamuuliza: “Ee Mtume wa Allaah, ikiwa atafanya haya ataingia Peponi?” Akasema: “Hakika hakuna muumini yeyote atakayepata sifa mojawapo ya hizi sifa isipokuwa itamshika mkono mpaka imuingize Peponi.”[3]
Ameipokea al-Bayhaqiy katika kitabu ”Shu‘ab-ul-Iymaan”.
´Umar bin al-Khatwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Nimetajiwa ya kwamba kitendo hujifakhari kati yao, swadaqah husema: ”Mimi ndiye bora wenu.”[4]
[1] al-Bukhaariy (1462) na Muslim (889).
[2] al-Bukhaariy (6539) na Muslim (1016).
[3] al-Bayhaqiy katika “Shu´b-ul-Iymaan” (6/502, 503, 504 na 506), at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” (6/156-157), Ibn Hibbaan (373) na al-Haakim (1/63), ambaye ameisahihisha kwa mujibuwa sharti za Muslim.
[4] al-Bayhaqiy katika “Shu´b-ul-Iymaan” (6/505) na al-Haakim (1/416), ambaye ameisahihisha kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 71-73
- Imechapishwa: 11/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 71-73
Imechapishwa: 11/08/2025
https://firqatunnajia.com/40-jikomboeni-nafsi-zenu-na-moto/