3 – Kifunguzi cha tatu cha swawm ni kula na kunywa kwa makusudi. Amesema (Ta´ala):
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ
“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]
Akahalalisha (Subhaanah) kula na kunywa mpaka kupambanuka kwa alfajiri ya pili, kisha akaamrisha kukamilisha funga mpaka usiku. Maana yake ni kuacha kula na kunywa katika kipindi kilicho kati ya kuchomoza alfajiri na kuingia usiku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesimulia kutoka kwa Mola wake kwamba amesema kuhusu mfungaji:
”Anaacha chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yake.”
Vilevile kufikisha kitu chochote cha majimaji au kigumu tumboni mwa mwenye kufunga, kama vile kuchukua sindano za lishe, kunywa dawa au kudungwa damu kwa ajili ya kumuokoa mwenye kufunga. Mambo haya yote huharibu swawm yake, kwa sababu ama ni vitu vya lishe vinavyosimama nafasi ya chakula. Kuhusu dawa zinazofika kooni na tumboni, nazo ziko katika hukumu ya chakula na kinywaji, kama walivyobainisha wanazuoni wengi (Rahimahumu Allaah). Ama sindano zisizo za lishe, ikiwa zinadungwa kwa njia ya mshipa, kinachoonekana ni kwamba zinamfunguza mfungaji kwa sababu huenda pamoja na damu na huingia tumboni. Ikiwa zinadungwa kwa njia ya misuli, basi tahadhari zaidi ni kuziacha. Hilo kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Acha kile chenye kukutia shaka na ukiendee kisichokutia shaka.”[2]
Yeyote anayehitaji kutumia kitu chochote katika haya yaliyotajwa kwa sababu ya maradhi yanayohitaji hilo na hayawezi kusubiri mpaka usiku, basi atumie na alipe siku hiyo, kwa kuwa yeye ni mgonjwa. Allaah amemruhusu mgonjwa kufungua na kulipa katika siku nyingine.
Baadhi ya wanazuoni wanazingatia kujipaka dawa ya macho kuwa ni miongoni mwa vifunguzi, kwa sababu inafika kooni na mara nyingi mwenye kufunga huhisi ladha yake kooni. Kwa hivyo haifai kwa mwenye kufunga kujipaka dawa ya macho mchana wa swawm, kwa kuchukua tahadhari na kujiepusha na shaka. Allaah ndiye anajua zaidi.
[1] 02:187
[2] an-Nasaa´iy (5727), Ahmad (01/200), Ibn ´Adiyy katika ”al-Kamaal” (01/203), at-Twabaraniy (32/285) na at-Tirmidhiy (2518) ambaye amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
al-Haythamiy amesema:
”Cheni yake ya wapokezi ni nzui.” (Majmaa´-uz-Zawaaid (04/74)).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 40-41
- Imechapishwa: 12/03/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 40-41
Imechapishwa: 12/03/2026
https://firqatunnajia.com/41-kula-na-kunywa-makusudi-kunamfunguza-mfungaji/