Inapendekezwa asome akiwa katika twahara. Akisoma hali ya kuwa hana wudhuu´ inajuzu kwa maafikiano ya waislamu, jambo ambalo Hadiyth katika hilo ni nyingi na zinajulikana. Imaam al-Haramayn amesema:
”Haisemwi kuwa ametenda jambo linalochukiza, bali yeye ameacha lililo bora zaidi. Ikiwa hakupata maji, basi atafanya Tayammum. Mwanamke mwenye damu ya ugonjwa (الإستحاضة) katika wakati unaohukumiwa kuwa ni twahara, hukumu yake ni kama mwenye hadathi.”
Ama mwenye janaba na mwenye hedhi, basi ni haramu kwao kusoma Qur-aan, ni mamoja iwe ni Aayah au chini ya hapo. Hata hivyo inajuzu kwao kuisoma Qur-aan kimyakimya moyoni bila kuitamka. Inajuzu kwao kuangalia msahafu na kuifikiria moyoni.
Waislamu wameafikiana juu ya kujuzu kumsabihi Allaah, kumpwekesha Allaah, kumhimidi Allaah, kumtukuza Allaah na kumswalia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa mujibu wa wafuasi wetu inajuzu kumwambia mtu:
يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ
”Ee Yahyaa! Chukua Kitabu kwa nguvu!”[1]
pasi na kukusudia kusoma Qur-aan. Wanaona pia kuwa inafaa kwao kusema wakati wa msiba:
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ
“Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake tutarejea.”[2]
Hata hivyo asikusudie kusoma Qur-aan. Wafuasi wetu kutoka Khurasaan wamesema kwamba inajuzu waseme wakati wa kupanda kipando:
سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ
“Utakasifu ni wa Yule ambaye ametutiishia haya na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti na hakika kwa Mola wetu bila shaka ni wenye kurejea!”[3]
na wakati wa kuomba du´aa:
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
“Mola wetu Tupe katika dunia mema na katika Aakhirah [pia Tupe] mema na tukinge na adhabu ya Moto!”[4]
Hata hivyo asikusudie kusoma Qur-aan. Imaam al-Haramayn amesema:
”Ikiwa mwenye janaba atasema:
بسم الله
“Kwa jina la Allaah.”
au:
الحمد لله
“Sifa njema zote njema anastahiki Allaah.”
ikiwa anakusudia kusoma Qur-aan atakuwa ametenda dhambi. Ikiwa anakusudia Dhikr au hakukusudia chochote, hatapata dhambi.”
Vilevile inajuzu kwao kusoma yaliyofutwa usomaji wake, kama vile:
الشيخ و الشيخة
“Mwanaume na mwanamke waliooa… ”
[1] 19:12
[2] 2:156
[3] 43:13-14
[4] 2:201
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 50
- Imechapishwa: 27/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 50
Imechapishwa: 27/08/2026
https://firqatunnajia.com/41-kujitwaharisha-kwa-ajili-ya-kusoma-qur-aan/