41. Ibn ´Uthaymiyn mgonjwa wa pumu kutumia sprei mchana wa Ramadhaan

Swali 41: Katika baadhi ya maduka ya dawa kunakuweko na sprei zinazotumiwa na baadhi ya wagonjwa wa pumu. Je, inafaa mfungaji kuitumia mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Inafaa kwa mfungaji kutumia sprei. Ni mamoja funga yake ikawa ni katika Ramadhaan au mwezi mwingine. Hayo ni kwa sababu sprei hii haifiki tumboni. Sprei hii hufika katika bronchi na ikafungua na baada ya hapo mtu akaweza kupumua upumuaji wa kawaida. Kwa hivyo jambo hilo halina maana ya kula na kunywa wala sio kula na kunywa kunakofika tumboni. Kama inavyofahamika msingi ni kusihi kwa swawm mpaka kupatikane dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah au kipimo sahihi inayojulisha juu ya uharibikaji.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 37
  • Imechapishwa: 28/04/2021