بسم الله الرحمن الرحيم
Huu hapa ni utafiti kuhusu kupangusa juu ya soksi za ngozi:
Tafiti ya kwanza inahusu kupangusa juu ya vitu vinavyofunika mguu ambavo vina matundu na vyembamba. Wanazuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Kwa mujibu wa maoni yaliyotangaa kwa Hanaabilah ni kwamba kupangusa juu yake hakusihi. Mtunzi wa “al-Muntahaa” amesema pindi alipokuwa anataja sharti za kupangusa:
“Isionyeshe ngozi ya mwili kutokana na wembamba au wepesi wake.”
Kabla ya hapo ametaja kwamba ni lazima ifunike yale maoneo ya mguu ambayo ni lazima kuyaosha.
Kitabu cha an-Nawawiy, “al-Majmuu´” ambacho ni kitabu cha Shaafi´iyyah, ametaja maoni mawili juu ya soksi za ngozi zilizo na matundu na kwamba maoni yaliyo sahihi zaidi ni kwamba asipanguse[1]. Kisha akataja namna ambavo Ibn-ul-Mundhir amemnukuu ath-Thawriy, Ishaaq, Yaziyd bin Haaruun na Abu Thawr ambao wamejuzisha kufuta juu ya soksi za ngozi aina zote. Ibn-ul-Mundhir amesema:
“Mi pia naonelea maoni hayo kwa sababu inavoonekana ni kana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliruhusu kupangusa juu ya soksi za ngozi zote, ndani yake kunaingia soksi za ngozi zote.”[2]
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema katika “al-Ikhtiyaaraat” kwamba inafaa kupangusa juu ya soksi za ngozi zenye matundu muda wa kuwa bado zinaitwa hivo na mtu anaweza kuzitembelea[3]. Haya ni maoni ya kitambo ya ash-Shaafi´iy na ni maoni ya Abul-Barakaat na wanazuoni wengine.
Ibn Hazm amesema katika “al-Muhallaa” kwamba inafaa kupangusa juu ya vitu vyenye kufunika mguu vilivyopasukapasuka hata kama itaonekana sehemu kubwa ya mguu muda wa kuwa bado kumebaki mguuni kitu katika sehemu yake. Amemnukuu Sufyaan ath-Thawriy kwamba amesema:
“Pangusa muda wa kuwa bado inaitwa “soksi za ngozi”.”[4]
Imekuja katika “al-Majmuu´” kwamba ni sawa kupangusa ile sehemu ya juu yenye matundu ikiwa sehemu ya ndani ni nzima. Vinginevyo haitofaa kwa sababu mguu utazingatiwa ni peku. Amesema:
“ar-Rawayyaaniy na ar-Raafi´iy wamenukuu njia ya ajabu na ambayo ni dhaifu inayojuzisha kupangusa hata kama ile sehemu ya ndani ni nyembamba.”[5]
Humo ametaja pia namna ambavo Ibn-ul-Mundhir amewanukuu Maswahabah tisa wenye kuonelea kufaa kupangusa juu ya soksi za kawaida. an-Nawawiy amesema:
“Wenzetu wamenukuu kutoka kwa ´Umar na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambao wamejuzisha kupangusa juu ya soksi za ngozi hata kama zitakuwa nyembamba. Pia wamenukuu hayohayo kutoka kwa Abu Yuusuf, Muhammad, Ishaaq na Daawuud.”[6]
Katika kitabu hichohicho ametaja pia kwamba inafaa kupangusa juu ya soksi za ngozi zinazoonyesha muda wa kuwa mtu anaweza kuzitembelea[7].
Katika kitabu ”Jawaahir-ul-Ikliyl Sharh Mukhtaswar Khaliyl” ametaja namna ambavo wamisri huita “soksi” soksi za ngozi zile ambazo ni aina ya pamba, sufu au kitu kingine[8].
[1] al-Majmuu´ (1/480).
[2] al-Majmuu´ (1/481).
[3] al-Ikhtiyaaraat, uk. 13.
[4] al-Muhallaa (2/100).
[5] al-Majmuu´ (1/482).
[6] al-Majmuu´ (1/484).
[7] al-Majmuu´ (1/486).
[8] Jawhar-ul-Ikliyl Sharh Mukhtaswar Khaliyl (1/24).
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/183-184)
- Imechapishwa: 07/05/2021

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/183-184)
Imechapishwa: 07/05/2021
https://firqatunnajia.com/40-tafiti-kuhusu-kupangusa-juu-ya-vitu-vinavyofunika-mguu-vyenye-mtundu-na-vyembemba/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)