Kuhusu idadi ya Rak´ah zake hakukuthibiti chochote kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni jambo lenye wasaa. Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Inafaa kwa mtu akaswali Rak´ah ishirini, kama ilivyotangaa katika madhehebu ya Ahmad na ash-Shaafi´iy, inafaa kwake kuswali Rak´ah thelathini na sita, kama yalivyo madhehebu ya Maalik, inafaa kwake kuswali Rak´ah kumi na moja au Rak´ah kumi na tatu, yote ni mazuri. Kwa hivyo kurefusha au kupunguzwa Rak´ah kunategemeaa urefu au ufupi wa kusimama.”[1]

´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipowakusanya watu nyuma ya Ubayy aliwaswalisha Rak´ah ishirini. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wako miongoni mwao walioswali Rak´ah chache na wako wengine walioswali Rak´ah nyingi. Kiwango maalum hakuna dalili kutoka katika Shari´ah.

[1] al-Akhbaar-ul-´Ilmiyyah min Ikhtiyaaraat-il-Fiqhiyyah, uk. 97.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/169)
  • Imechapishwa: 07/05/2021