40. Kuna neno mtu akifunga swawm iliyopendekezwa siku ya jumamosi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kufunga swawm iliyopendekezwa siku ya jumamosi? Je, swawm ya mtu inaathirika akiulizwa kama amefunga akaitikia? Je, inafaa kusema kuwa hakufunga ikiwa anachelea kujionyesha?

Jibu: Imechukizwa kufunga jumamosi peke yake. Mtu asifunge jumamosi kama hakunuia kufunga pamoja nayo siku moja kabla au baada yake. Kuhusu kuipwekesha ni jambo lisilotakikana. Hata hivyo hapana neno kufunga jumamosi peke yake ikiwa mtu analipa deni la Ramadhaan, imekutana na siku ya ´Arafah au siku ya ´Aashuuraa´. Kinachochukizwa ni kuipwekesha jumamosi ikiwa funga hiyo ni ya kujitolea.

Kuhusu mtu akimuuliza mfungaji, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu akimtukana au akampiga vita, basi aseme: “Mimi nimefunga, mimi nimefunga.”[1]

Asisemi kuwa amefunga isipokuwa pale ambapo mtu atamfanyia ujinga. Lakini ikiwa mtu anakuuliza kwa sababu anataka kukualika chakula au kinywaji na ukajibu kuwa umefunga au ukamjibu kuwa umefunga kwa sababu ya kumbainishia kuwa kuacha kwako kitu hicho sio kwa sababu ya kukichukia, hakuna neno. Nataraji kuwa sio kujionyesha.

[1] al-Bukhaariy (1904) na Muslim (1151).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 04/04/2022