40. Dalili ya Jahmiyyah kwamba Allaah yuko kila mahali

Ubainifu juu ya tafsiri ya Jahmiyyah ya maneno Yake Allaah:

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ

”Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao.”[1]

Wanasema kuwa Allaah yuko pamoja nasi na ndani yetu. Allaah ameanza kusema:

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ

“Je, huoni kwamba Allaah anajua yale yote yaliyomo mbinguni na yale yote yaliyomo ardhini?”

Kisha akasema:

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمٌْ

”Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao… ”

Bi maana kwa utambuzi Wake.

وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ

”… na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao… ”

Bi maana kwa utambuzi Wake.

وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا

”… na wala [hauwi mnong’ono wa] chini kuliko ya hivyo, na wala wa wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa.”

Bi maana kwa utambuzi Wake juu yao.

ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

”Kisha siku ya Qiyaamah atawajuza yale waliyoyafanya. Hakika Allaah kwa kila jambo ni Mjuzi.”[2]

Ameyaanza maelezo kwa ujuzi Wake na akayamaliza maelezo kwa ujuzi Wake.

Muulize swali lifuatalo Jahmiy huyu: Ikiwa Allaah yuko pamoja nasi kwa utukufu Wake, je, anakusameheni katika yale yaliyoko kati Yake na viumbe Wake? Akisema ndio, basi atakuwa amedai kuwa Allaah ametengana na viumbe Wake. Akisema hapana, anakufuru[3].

[1] 58:7

[2] 58:7

[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 29/04/2024