Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Amekuamrisheni kutoa swadaqah. Hakika mfano wa hilo ni mfano wa mtu aliyetekwa na adui ambapo wakamfunga mikono yake… ”[1]
Haya pia ni katika maneno ambayo dalili yake ni kuwepo kwake. Ushahidi wake ni kutokea kwake, kwani hakika ya swadaqah ina athari ya ajabu katika kuondoa aina mbalimbali za majanga, hata ikiwa ni kutoka kwa fasiki, dhalimu au hata kafiri. Kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) humuepusha nayo aina mbalimbali za mabalaa, jambo ambalo linalojulikana vyema kwa watu wote. Watu wote wa ardhini wanalikubali kwa sababu wamelijaribu. Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika ya swadaqah huzima ghadhabu ya Mola na huzuia kifo kibaya.”
Ameipokea at-Tirmidhiy.
Kama inavyozima ghadhabu ya Mola (Tabaarak wa Ta´ala), basi huzima madhambi na makosa kama vile maji yanavyozima moto. Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
“Nilikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika safari. Nikawa karibu naye siku moja na sisi twatembea ambapo akaniambia: ”Je, nisikujulishe milango ya kheri? Kufunga ni ngao na swadaqah huzima makosa kama maji yanavyozima moto na swalah ya mtu ndani ya usiku wa kati ni alama ya watu wema.” Kisha akasoma:
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ
“Mbavu zao zinatengana na vitanda wakimuomba Mola wao kwa khofu na matumaini na katika yale tuliyowaruzuku wanatoa.”[2]
Imekuja katika baadhi ya masimulizi:
”Fanyeni haraka kutoa swadaqah, kwani bala haipitii swadaqah.”[3]
[1] at-Tirmidhiy (664), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni. Sehemu yake ya kwanza ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (664).
[2] 32:16-17
[3] at-Tirmidhiy (2616), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (983).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 69-71
- Imechapishwa: 11/08/2025
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Amekuamrisheni kutoa swadaqah. Hakika mfano wa hilo ni mfano wa mtu aliyetekwa na adui ambapo wakamfunga mikono yake… ”[1]
Haya pia ni katika maneno ambayo dalili yake ni kuwepo kwake. Ushahidi wake ni kutokea kwake, kwani hakika ya swadaqah ina athari ya ajabu katika kuondoa aina mbalimbali za majanga, hata ikiwa ni kutoka kwa fasiki, dhalimu au hata kafiri. Kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) humuepusha nayo aina mbalimbali za mabalaa, jambo ambalo linalojulikana vyema kwa watu wote. Watu wote wa ardhini wanalikubali kwa sababu wamelijaribu. Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika ya swadaqah huzima ghadhabu ya Mola na huzuia kifo kibaya.”
Ameipokea at-Tirmidhiy.
Kama inavyozima ghadhabu ya Mola (Tabaarak wa Ta´ala), basi huzima madhambi na makosa kama vile maji yanavyozima moto. Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
“Nilikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika safari. Nikawa karibu naye siku moja na sisi twatembea ambapo akaniambia: ”Je, nisikujulishe milango ya kheri? Kufunga ni ngao na swadaqah huzima makosa kama maji yanavyozima moto na swalah ya mtu ndani ya usiku wa kati ni alama ya watu wema.” Kisha akasoma:
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ
“Mbavu zao zinatengana na vitanda wakimuomba Mola wao kwa khofu na matumaini na katika yale tuliyowaruzuku wanatoa.”[2]
Imekuja katika baadhi ya masimulizi:
”Fanyeni haraka kutoa swadaqah, kwani bala haipitii swadaqah.”[3]
[1] at-Tirmidhiy (664), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni. Sehemu yake ya kwanza ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (664).
[2] 32:16-17
[3] at-Tirmidhiy (2616), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (983).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 69-71
Imechapishwa: 11/08/2025
https://firqatunnajia.com/39-swadaqah-dhidi-ya-mabalaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket