Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Isitoshe yanapatikana pia katika Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio yenye kuifasiri Qur-aan, kuibainisha, kuifahamisha na kuiweka wazi. Vilevile ni wajibu kuamini yale Mtume aliyomsifu kwayo Mola Wake (´Azza wa Jall) kutokana na zile Hadiyth Swahiyh ambazo zimekubaliwa na wanazuoni. Ni miongoni mwa hayo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mola Wetu huteremka katika mbingu ya chini kila usiku pale kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na akasema: “Ni nani mwenye kuniomba nimjibie? Ni nani mwenye kuniuliza nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?”[1]
”Allaah hufurahishwa zaidi na tawbah ya mja wake zaidi kuliko vile anavyofurahi mmoja wenu pale anapomkosa ngamia wake ambaye yuko na chakula na kinywaji chake juu yake. Kisha akamtafuta na asimpate. Baada ya hapo akalala chini ya mti na huku akisubiria kifo. Tahamaki ngamia yule amesimama juu yake. Akamshika khatamu na kwa furaha nyingi akasema: ”Ee Allaah! Wewe ni mja wangu na mimi ndiye Mola Wako.”[2]
“Allaah anawacheka watu wawili ambapo mmoja wao kamuua mwenzake. Halafu wote wawili wanaingia Peponi.”[3]
“Anastaajabu Mola Wetu kwa kukata tamaa waja Wake licha ya mabadiliko Yake ya hali zao yako karibu. Huwatazama mnapokuwa katika hali ngumu na wenye kukata tamaa. Huanza kucheka kwa kuwa Anajua kuwa faraja yenu iko karibu.”[4]
Hadiyth ni nzuri.
“Haitoacha Jahannam kutupwa ndani yake [watu na mawe] nayo inasema:
هَلْ مِن مَّزِيدٍ
“Je, kuna zaidi?” (50:30)
mpaka Mola Mtukufu (Tabaarak wa Ta´ala) aweke Mguu Wake – na imekuja katika upokezi mwingine “unyayo Wake” juu yakwe kisha pawe sawa. Hapo ndio itasema “Inatosha! Inatosha!”[5]
“Allaah (Ta´ala) atasema: “Ee Aadam!” Atajibu: “Ninaitikia wito Wako na nakuomba unifanye ni mwenye furaha na mafanikio.” Kisha Ataita kwa sauti: “Hakika Allaah anakuamrisha utoe moja katika kizazi chako Motoni.””[6]
MAELEZO
Hadiyth hizi sita ni kama Aayah zilizo kabla yake. Ni kama jinsi Qur-aan inavyofahamisha kuthibitisha sifa na majina kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kwamba Yeye (Jalla wa ´Alaa) anaitwa kwa majina mazuri kabisa na anasifika vilevile kwa sifa kuu. Kama ambavyo imekuja katika Qur-aan kadhalika imekuja katika Sunnah. Hakika ya Sunnah Swahiyh za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinaifasiri Qur-aan, kuibainisha na kuiweka wazi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ
“Hakika si vyenginevyo waumini ni wale waliomwamini Allaah na Mtume Wake… ” (24:62)
أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ
“Mtiini Allaah na mtiini Mtume.” (04:59)
وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ
“Naapa kwa nyota inapotua! Hakupotea sahibu yenu na wala hakukosea. Na wala hatamki kwa matamanio yake – hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa.” (53:01-04)
Kama ambavyo kumekuja Aayah zenye kuzungumzia sifa na majina ya Allaah na Sunnah imefanya vivyo hivyo. Yaliyothibiti ndani ya Sunnah Swahiyh hukumu yake ni kama ile iliyothibiti ndani ya Qur-aan. Kwa hivyo itakuwa ni wajibu kumthibitishia nayo Allaah na kuamini kuwa ni sifa na majina ya Allaah kwa njia inayolingana Naye (Subhaanah) pasi na kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna na kulinganisha. Mlango na hukumu ni moja. Yaliyokuja katika Sunnah Swahiyh hukumu yake ni kama yaliyokuja katika Qur-aan. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa yote ni sawasawa. Kwa mfano maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mola Wetu huteremka katika mbingu ya chini kila usiku pale kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na akasema: “Ni nani mwenye kuniomba nimjibie? Ni nani mwenye kuniuliza nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?” mpaka kupambazuke.”
Ahl-us-Sunnah wanamthibitishia Allaah sifa ya ushukaji huu. Ni ushukaji unaolingana na Allaah. Hafanani na viumbe Wake katika ushakaji Wake. Kiumbe yeye kwa mfano hushuka kutoka juu na kwenda chini na kutoka juu ya mlima na kwenda chini, lakini hata hivyo ushukaji wa Allaah sio kama ushukaji wa kiumbe. Ushukaji mmoja ni tofauti na ushukaji mwingine.
[1] al-Bukhaariy (7494) na Muslim (758).
[2] al-Bukhaariy (6308) na (2747).
[3] al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890).
[4] Ibn Maajah (181). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (2810).
[5] al-Bukhaariy (4848) na Muslim (2846).
[6] al-Bukhaariy (7483) na Muslim (222).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 55-57
- Imechapishwa: 23/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 55-57
Imechapishwa: 23/10/2024
https://firqatunnajia.com/39-msimamo-wa-ahl-us-sunnah-juu-ya-majina-na-sifa-za-allaah-katika-sunnah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)