39. Kuwasomea al-Ikhlaasw wafu mara kumi na moja

Swali: Imepokelewa kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayepita makaburini na akasoma:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.”[1]

mara kumi na moja kisha malipo yake akawapa zawadi wale wafu, basi atapewa thawabu kwa idadi ya wale wafu. Je, Hadiyth hii ni Swahiyh?

Jibu: Hadiyth hii haina msingi kwa kwa wanazuoni. Ni miongoni mwa Hadiyth zilizozuliwa na za uwongo ambazo hazina mategemezi Swahiyh. Si katika Sunnah kusoma kwenye kaburi wala kujenga juu yake. Sunnah kwa anayeyatembelea makaburi aseme:

السلام عليكم دار قوم مؤمنين

“Amani ya Allaah iwe juu yenu wakazi waumini… “

au:

السلام عليكم أهل الديار من المؤمنين والمسلمين وإنا إن شاء الله بكم لاحقون نسأل الله لنا ولكم العافية يرحم الله المستقدمين منا والمستأخرين

“Amani ya Allaah iwe juu yenu wakazi waumini na waislamu. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana na nyinyi. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi afya. Allaah amrehemu aliyetangulia katika sisi na atakayekuja baadaye.”[2]

Halafu awaombee du´aa ya msamaha na rehema. Hii ndio Sunnah. Ama kuwasomea Qur-aan au Qur-aan kati yao ni kitu hakina msingi.

[1] 112:01

[2] Muslim (974).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 20/07/2022