Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Katika kiwanja cha Mkusanyiko wa Qiyaamah kutakuwa hodhi iliyotajwa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maji yake ni meupe mno kuliko maziwa na matamu zaidi kuliko asali. Vikombe vyake ni wingi wa idadi ya nyota mbinguni. Urefu na upana wake ni sawa na mwendo wa mwezi. Anayekunywa humo mara moja, hatopata kiu baada yake kamwe.
MAELEZO
Huu ni utafiti wenye kuzungumzia kuhusu hodhi na Njia. Hodhi hii itakuwa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ndio ile iliyoitwa al-Kawthar:
إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ
“Hakika Sisi Tumekupa [mto wa] al-Kawthar!” (108:01)
Inamimina humo kutoka kwenye Kawthar. Vinginevyo Kawthar iko Peponi. Hodhi hii imewekewa mifereji miwili kutoka kwenye aKawthar.
Hodhi hii itakuwa duniani ardhini na imewekewa mifereji miwili kutoka Kawthar. Ni hodhi itaendewa na waumini ambao ni wafuasi wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Urefu wake ni mwezi na upana wake ni mwezi. Vikombe vyake ni sawa na idadi ya nyota mbinguni. Maji yake ni meupe zaidi kushinda maziwa na ladha yake ni matamu zaidi kushinda asali. Mwenye kunywa humo basi hatohisi kiu kamwe mpaka pale atapoingia Peponi. Waumini wataufikia na kunywa ndani yake. Hili linahusiana na wale wafuasi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna watu ambao watafukuzwa. Kisha ataulizwa Mola ambapo atasema:
“Hakika hawa walibaki ni wenye kuritadi tangu ulipofarakana nao.”
Kwa hivyo watazuia kuifikia. Baada ya hapo aseme (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Atokomee! Atokomee yule aliyebadilisha baada yangu!”[1]
Hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa hodhi hii itaendewa tu na waumini ambao wamekufa na hali ya kuwa wanamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanafuata dini yake. Kuhusu walioritadi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), au wakati mwingine wowote, hawa hawatoifikia hodhi hii. Vilevile inahusiana na makafiri wengine wote hawatoweza kuifikia hodhi hii. Wataifikia tu waumini miongoni mwa wafuasi wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Mitume wengine (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) nao pia watakuwa na hodhi zao[2]. Lakini hata hivyo hodhi yake yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kamilifu na yenye kutimia zaidi. Watafukuzwa kwenye hodhi yake wasiokuwa katika kizazi chake kama inavyofukuzwa ngamia ngeni. Hakuna watayoifikia isipokuwa tu wale waumini ambao ni wakweli. Ama walioritadi hawana fungu kwayo. Hakuna hila wala nguvu isipokuwa kwa Allaah. Tunamuomba Allaah sote atujaalie kuwa miongoni mwa wataoifikia.
[1] al-Bukhaariy (4625) na Muslim (2860).
[2] at-Tirmidhiy (2443). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyh” (1589).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 88-90
- Imechapishwa: 28/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 88-90
Imechapishwa: 28/10/2024
https://firqatunnajia.com/39-itiqaad-ya-ahl-us-sunnah-wal-jamaaah-juu-ya-hodhi-na-njia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)