Mlango huu ndio kusudio la kitabu. Umeenea sana, kwa ajili hiyo ninaashiria baadhi ya pande za makusudio yake kwa kuchukia kurefusha na kwa kumkhofia msomaji wake kuchoka.

Jambo la kwanza katika hilo ni kwamba ni lazima kwa msomaji amtakasie nia Allaah, kama tulivyotangulia kusema, na kuzingatia adabu na Qur-aan. Inampasa afikirie kuwa anamsemesha Allaah (Ta´ala) na anasoma katika hali ya kumuona Allaah (Ta´ala). Kwa sababu ikiwa hamuoni, basi Allaah (Ta´ala) anamuona.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 49
  • Imechapishwa: 26/08/2026